Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Pendekezo la serikali la kuongoza kwa miaka kumi lafutiliwa mbali nchini Mali

Nchini Mali, uamuzi wa kuongezwa kwa serikali ya mpito kuendelea kuongoza kwa miaka mitano, unaendelea kushtumiwa na wadau mbalimbali.

Assimi Goita, rais wa mpito nchini Mali.
Assimi Goita, rais wa mpito nchini Mali. AFP - ANNIE RISEMBERG
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa vyama 100 vya siasa na mashirika 60 ya kiraia, yanapinga pendekezo hilo na unataka uongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kuendelea kushinikiza uongozi wa kijeshi kuandaa uchaguzi huo haraka.

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wanatarajiwa kukutana juma hili, kuzungumza kuhusu mapendekezo yaliyowasilishwa na Serikali ya mpito ya Mali.

Haya yanajiri baada ya siku ya Ijumaa, wadau wa kisiasa nchini Mali, walioshiriki kongamano la kitaifa la kuijenga upya Mali, kupendekeza serikali iliyopo sasa kuongezewa muda wa miaka metano.

Hata hivyo mapendekezo haya ya Mali, huenda yasipokelewe vizuri na wakuu wa nchi za ECOWAS ambao waliipa nchi ya Mali hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu kutoa kalenda na kufanya uchaguzi mkuu.

Serikali ya mpito ya Mali inasema muda uliotolewa na ECOWAS hautoshi kufanya mabadiliko yanayotakiwa na raia wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.