Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

ECOWAS kujadili mapendekezo ya Serikali ya mpito ya Mali

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wanatarajiwa kukutana juma lijalo, kuzungumza kuhusu mapendekezo yaliyowasilishwa na Serikali ya mpito ya Mali.

Wakuu wa nchi za ECOWAS ambao waliipa nchi ya Mali hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu kutoa kalenda na kufanya uchaguzi mkuu.
Wakuu wa nchi za ECOWAS ambao waliipa nchi ya Mali hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu kutoa kalenda na kufanya uchaguzi mkuu. © RFI/Serge Daniel
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri baada ya siku ya Ijumaa, wadau wa kisiasa nchini Mali, walioshiriki kongamano la kitaifa la kuijenga upya Mali, kupendekeza serikali iliyopo sasa kungezewa muda wa miaka metano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop, amesema tayari Serikali yao imewasilisha mapendekezo hayo kwa wakuu wa nchi za ECOWAS ambao watakutana kujadili ikiwa wakubali au la.

 Hata hivyo mapendekezo haya ya Mali, huenda yasipokelewe vizuri na wakuu wa nchi za ECOWAS ambao waliipa nchi ya Mali hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu kutoa kalenda na kufanya uchaguzi mkuu.

Serikali ya mpito ya Mali inasema muda uliotolewa na ECOWAS hautoshi kufanya mabadiliko yanayotakiwa na raia wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.