Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Ujumbe wa Mali kukutana na ECOWAS, baada ya mashauriano ya kitaifa

Ujumbe wa Mali unatarajiwa kwenda Accra kuripoti kuhusu mshauriano ya kitaifa kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Mgharibi, ECOWAS, Nana Akufo-Addo, rais wa Ghana.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, Mwenyekiti wa sasa wa ECOWAS. Paul Marotta/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop. Hakuna taarifa rasmi kuhusu mpango huu lakini, kulingana na chanzo cha serikali, wajumbe walitarajia kuongoka Bamako Ijumaa hii, Desemba 31. Kuna uharaka kwa vile ECOWAS ilikuwa imetoa kauli ya mwisho huko Bamako. Bila utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na mamlaka ya mpito kwa kuandaa chaguzi zijazo, vikwazo vya kiuchumi vitachukuliwa kuanzia tarehe 1 Januari.

Hayo yanajiri wakati maoni mbalimbali yameendelea kutolewa baada ya Tume maalum iliyokuwa inakusanya maoni kuhusu mustakabali wa nchi hiyo kutoa ripoti yake baada ya jeshi kuchukua madaraka mwaka uliopita.

Pendekezo la serikali ya mpito inayoongozwa na Kanali Asimi Goita la kuongezwa kipindi kilio kati ya miezi sita mpaka miaka mitano kwa sababu za kiusalama, kumepingwa vikali na vyama vya upinzani.

Miongoni mwa mapendekezo mengine ambayo yamependekezwa ni pamoja na ujenzi wa kambi mpya za jeshi, kuimarisha jeshi, kuwepo kwa katiba mpya na kupambana na ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.