Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Somalia: Juimuiya ya kimataifa watoa wito wa mazungumzo kati ya Waziri Mkuu na rais

Hali bado si shwari nchini Somalia ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka kati ya Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble na Rais Farmajo. Kutokana na mivutano hii, jumuiya ya kimataifa imeongeza kutoa wito wa mazungumzo.

Uhusiano si mzuri kati ya Rais Farmajo na Waziri wake Mkuu. Jumuiya ya kimataifa inatoa wito wa utulivu na mazungumzo.
Uhusiano si mzuri kati ya Rais Farmajo na Waziri wake Mkuu. Jumuiya ya kimataifa inatoa wito wa utulivu na mazungumzo. - AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mzozo kati ya rais wa Somalia na waziri wake mkuu wake unaendelea. Wiki moja iliyopita Rais Farmajo alijaribu kumsimamisha kazi Waziri wake Mkuu , Mohamed Hussein Roble, kutokana na tuhuma za rushwa. Hata hivyo Mohamed Hussein Roble alimjibu akimshutumu kutaka kujipatia madaraka. Wawili hawa wamekuwa katika mvutano kwa miezi kadhaa kuhusiana na uchaguzi, ambao ni kinyume na muda uliopangwa.

Katika mabadiliko ya hivi punde hadi sasa, Waziri Mkuu alitangaza Jumamosi jioni (Januari 1) kuundwa kwa kamati ya mawaziri kuchunguza jaribio la kumwondoa madarakani. Upinzani unamtaka rais ajiuzulu.

Jumuiya ya kimataifa inataka mazungumzo

Hali inatia wasiwasi zaidi kwani kila kambi inanufaika na usaidizi ndani ya vikosi vya usalama. Jumuiya ya kimataifa imeongeza kutoa wito wa kutuliza pande hizombili. Siku ya Alhamisi, Desemba 30, Umoja wa Afrika uliwaalika watu hao wawili kwenye mazungumzo na kutafuta suluhu la kisiasa la mgogoro huo.

Marekani na Uingereza zilisisitiza udharura wa kukamilisha mchakato wa uchaguzi. Nchi hizo mbili pia zimeonyesha kuunga mkono kufanyika kwa baraza la kitaifa kuhusu uchaguzi, lililopendekezwa na Mohamed Roble.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.