Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Mgogoro wa kisiasa nchini Somalia: Mvutano waongezeka Mogadishu

Baada ya Waziri Mkuu kufukuzwa kazi na mkuu wa nchi, hali ni tete nchini Somalia. Jumanne hii asubuhi, wanajeshi wenye silaha nzito wametumwa katika maeneo ya kimkakati ya mji mkuu.

Wanajeshi wanaomuunga mkono Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble wakipanda katika magari yao wakati wajikusanya katika kijiji cha Siigale katika wilaya ya Hodan huko Mogadishu,  Somalia, Desemba 27, 2021.
Wanajeshi wanaomuunga mkono Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble wakipanda katika magari yao wakati wajikusanya katika kijiji cha Siigale katika wilaya ya Hodan huko Mogadishu, Somalia, Desemba 27, 2021. REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Tangu asubuhi hii, wanajeshi walio na silaha nzito watiifu kwa Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble wamepiga kambi katika maeneo yanayozunguka ikulu ya rais. Wamejihami kwa silaha kali, kulingana na mashahidi.

Madhumuni ya kutumwa kwa wanajeshi hao bado haijulikani, lakini inajiri saa chache baada ya mkuu wa nchi, Rais Farmajo, kujaribu kumtimua waziri mkuu. Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble alishutumu kile alichokiita "jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali" na kuwataka wakuu wa vikosi vya usalama kuchukua maagizo yao kutoka kwake na sio kutoka kwa rais.

Katika muktadha huu, na hata ikiwa kwa sasa jiji liko shwari, lukata hizi za kijeshi zinazua hofu ya mlipuko wa vurugu. Tangu Jumatatu, viongozi kadhaa wa kisiasa na viongozi wa kimila wamejaribu kushiriki katika majadiliano na kambi hizo mbili ili kutatua mgogoro huo.

Kwa sababu ikiwa mvutano huo unajirudia kati ya wawili hao, unaonekana kushika kasi tangu Jumatatu. Washirika wa Somalia, sawa na baadhi ya nchi 20 na mashirika ya kimataifa, pia wameelezea wasiwasi wao katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Pia washirika hao wanaoana kama kero mzozo huu wa kisiasa ambao unazidi kuzorota na ambao unahatarisha kudhoofisha zaidi Somalia katika kukabiliana na tishio kutoka kwa wanamgambo wa Kiislamu wa Al shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.