Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Somalia: Rais Farmajo 'amsimamisha' kazi Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi, anayejulikana kwa jina la Farmajo, alitangaza katika taarifa usiku wa Jumapili 26 kuamkia Jumatatu Desemba  27 kwamba "amemuachisha kazi" Waziri Mkuu wake Mohamed Hussein Roble "kufuatia madai ya rushwa" . Wawili hao wako kwenye mvutano kuhusu kufanyika kwa uchaguzi na ambao utapelekea kuteuliwa kwa rais mpya wa nchi.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, almaarufu Farmajo, hapa alikuwa New York, Septemba 23, 2019.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, almaarufu Farmajo, hapa alikuwa New York, Septemba 23, 2019. Riccardo Savi / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu alituhumiwa siku chache zilizopita na kamanda wa kikosi cha ulinzi wa pwani, rafiki wa karibu wa rais Mohamed Abdullahi, kutumia fursa ya kupokonya ardhi ya jeshi la wanamaji, tuhuma iliyofutiliwa mbali vikali na mhusika na mawaziri kadhaa waliohusishwa kwa madai hayo. Taarifa kutoka Villa Somalia inabaini jaribio la Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi kuingilia uchunguzi uliofunguliwa na jeshi kuhusu tuhuma hizi.

Licha ya kusimamishwa kazi kwa Waziri Mkuu, taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa wajumbe wengine wa serikali "wataendelea kutekeleza majukumu yao".

Katika taarifa ya pili dakika chache baadaye, rais pia "aliagiza" kusimamishwa kazi kwa kamanda wa jeshi la wanamaji la Somalia, Brigedia Jenerali Abdihamid Mohamed Dirir.

Mgogoro kati ya watu hao wawili unatokana na hatima ya uchunguzi wa mazingira tatanishi ya kutoweka kwa Ikran Tahlil Farah, afisa wa idara ya ujasusi, mwezi Juni mwaka huu. Waziri Mkuu alikataa uchunguzi ndani wa kijasusi, akiwashutumu wanajihadi wa Al Shabab, na kumfukuza mkurugenzi wake. Hayo yalijiri wakati familia ya mwathiriwa ikishutumu waziwazi kiongozi wa Ikran Tahlil Farah, ambaye ofisi ya rais ilikuwa ikimlinda.

Suala hili nyeti litashughulikiwa na mahakama za kiraia, na sio tume ya uchunguzi kama ilivyoagizwa na Waziri Mkuu au na mahakama ya kijeshi kama anavyotaka rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.