Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Washirika wa Somalia watiwa wasiwasi na mgogoro katika serikali

Washirika wa Somalia wameelezea wasiwasi wao kufuatia malumbano kati ya rais wa nchi hiyo Mohamed Farmajo na Waziri wake Mkuu Mohamed Hussein Roble.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed (kushoto). Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble (kulia).
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed (kushoto). Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble (kulia). AFP - YASUYOSHI CHIBA,ABDIRAHMAN YUSUF
Matangazo ya kibiashara

Hayo ni baada ya Rias Mohamed Farmajo kutangaza usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Desemba 27 kumuachisha kazi Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble, kufuatia madai ya "ufisadi".

Wawili hao wamekuwa katika mzozo kwa miezi kadhaa kuhusu suala la mzunguko wa uchaguzi, ambao umekwama. Lakini Waziri Mkuu amekataa kutii sheria hiyo na kudai kwamba rais Mohamed Farmajo amepoteza haki zake za kikatiba. Washirika wa Somalia wanaelezea wasiwasi wao na wanakerwa na hali hiyo.

Saa chache baada ya kusimamishwa kazi na mkuu wa nchi siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble alirejea katika ofisi yake, akiwa amezungukwa na wajumbe wa baraza lake la mawaziri, mkuu wa jeshi na wanajeshi, huku wapiganaji wanaomuunga mkono wakijitokeza mjini kwenye magari yao.

Aliwahutubia wafuasi wake akishutumu "jaribio la kuipindua" serikali. "Uchaguzi, ndio, mapinduzi ya kijeshi, hapana," alipiga, akimtaja Mohamed Farmajo kuwa "hatari kwa utulivu wa nchi" na kuwataka wakuu wa vikosi vya usalama kuchukua maagizo kutoka kwake, na hapana kutoka kwa rais.

Katika taarifa, washirika wa Somalia, sawa na baadhi ya nchi ishirini na mashirika ya kimataifa, wameelezea wasiwasi wao na kutaka kujizuia kutoka kwa viongozi wa Somalia, wakiwataka "kuepuka uchochezi au matumizi ya nguvu", na kutoa wito kwa mara nyingine wa kuendeleza mzunguko wa uchaguzi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.