Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Waandamanaji wakasirishwa na hatua ya hamdok kukubali kurejeshwa kwenye wadhifa wake

Waziri Mkuu wa Sudan Abdulla Hamdok aliyerejeshewa madaraka na jeshi ameapa kuunda serikali ya watalaam, anaosema watasaidia nchi hiyo kurejea kwenye uongozi wa demokrasia, mwezi mmoja baada ya jeshi kuchukua madaraka.

Waanamanaji wanaopinga mainduzi ya kijeshi wameapa kuendelea na maandamano licha ya Hamdok kurejeshwa kwenye wadhifa wake wa waziri mkuu;
Waanamanaji wanaopinga mainduzi ya kijeshi wameapa kuendelea na maandamano licha ya Hamdok kurejeshwa kwenye wadhifa wake wa waziri mkuu; - AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano maalum na Televisheni ya Al Jazeera, ambaye amerejeshewa madaraka baada ya kusaini makubaliano na jeshi, amesema serikali atakayoiunda, itakuwa huru.

Aidha, amesema kazi kubwa itakayofanywa na serikali yake inayoundwa kwa sasa, ni kuhakikisha kuwa inafanikisha kuwepo kwa mazungumzo kuhusu katiba mpya, lakini pia kuhakikisha kuwa Uchaguzi unafanyika ifikapo Juni mwaka 2023.

Jumapili iliyopita, kulikuwa na maandmaano makubwa kupinga makubaliano kati ya Hamdok na uongozi wa kijeshi.

"Inasikitisha. Hatukutarajia hili kutoka kwa Hamdok. Alikuwa siku zote upande wetu na kuunga mkono harakati zetu, lakini ameturudisha nyuma kwa kuungana na Al Burhan, ameachana na madai ya waandamanaji", mmoja wa wandamanaji ameelezea masikitiko yake.

Mwandamanaji mwingine anataka kiongozi wa kijeshi Jenerali afunguliwe mashtaka baada ya kuuawa kwa waandamanaji.

Watu 40 wameuawa. Iwapo Burhan atakubali kufunguliwa mashtaka,hatuna shida ya kuzungumza na jeshi, lakini tunapinga kabisa makubaliano haya kwa sababu hatuliamini tena jeshi. Tunachoataka sisi ni serikali ya kiraia kwa asilimia 100. Sio Hamdok, Burhan wala Hamdok watakaobadilisha mawazo yetu.

Maandamano zaidi yanatarajiwa kushuhudiwa katika siku zijazo, baada ya makubaliano kati ya Jeshi na Hamdok, ikiwa ni pamoja na kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.