Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Wingu latanda kwenye makubaliano kati ya Abdallah Hamdok na Jenerali Al-Burhan

Abdallah Hamdok kwa mara nyingine tena anashikilia wadhifa wake kama Waziri Mkuu wa Sudan. Alirejeshwa kwenye wadhifa wake jana kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini na Jenerali Burhan, kiongozi mkuu wa mapinduzi ya Oktoba 25. Lakini vuguvugu linalopinga mapinduzi limefutilia mbali makubaliano yoyote na Jenerali Burhan na limesema litaendelea na maandamano kutetea demokrasia.

Jenerali Al-Burhane katika mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Mei 17, 2021.
Jenerali Al-Burhane katika mkutano na waandishi wa habari huko Paris, Mei 17, 2021. © REUTERS/Sarah Meyssonnier/Pool/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Takriban mwezi mmoja baada ya mapinduzi hayo, wawili hao wanaahidi kuzindua upya mageuzi ya kidemokrasia ambayo yanatarajiwa kuwezesha mchakato wa uchaguzi na kukabidhi mamlaka kwa raia.

Kurejeshwa kwa Abdallah Hamdok kwenye wadhifa wake, kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa na kurejea kwa mgawanyo wa madaraka kati ya wanajeshi na raia: haya ndiyo masharti yaliyowekwa na jumuiya ya kimataifa kuendelea kuiunga mkono Sudan.

Kwa mtazamo huu, makubaliano yaliyofikiwa jana kwa hivyo yanamruhusu Jenerali Burhan kuvunja mkwamo ambao mapinduzi yake ya kijeshi yalikuwa yameweka.

Kwa hakika makubaliano haya yananachukua kama mfumo wa marejeleo ya kutangazwa kwa katiba, tamko lililotiwa saini mwanzoni mwa kipindi cha mpito lakini yanaeleza kwamba nakala hii italazimika kurekebishwa ... bila maelezo zaidi. Nakala ambayo Jenerali Al-Burhan pia alikiuka na kurekebisha hivi majuzi, hasa ili kuwatenga vuguvugu lililotetea Uhuru na Mabadiliko.

Aidha, mkataba huo hauelezi tarehe ya uchaguzi ujao, wala hautoi uamuzi kuhusu - suala kuu la kukabidhi raia nafasi ya uongozi wa Baraza Kuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.