Pata taarifa kuu
ETHIIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Serikali yaadai kutwaa miji ya Dessie na Kombolcha

Nchini Ethiopia, serikali ya shirikisho inaendelea kusonga mbele kaskazini mwa nchi. Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imehakikisha, Jumatatu hii, Desemba 6, kuwa imetwaa miji ya Dessie na Kombolcha, miji miwili ya zaidi ya wakazi 200,000. Wakati waasi wa TPLF Tigray walikuwa kilomita 180 kutoka mji mkuu Addis Ababa, siku kumi zilizopita, walianza kuondoka hadi eneo la Tigray.

Hivi karibuni Waziri Mkuuu Abiy Ahmed aliapa kuangamiza kundi la waasi wa TPLF? kama hawatakubali kujisalimisha.
Hivi karibuni Waziri Mkuuu Abiy Ahmed aliapa kuangamiza kundi la waasi wa TPLF? kama hawatakubali kujisalimisha. © Twitter/Abiy Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Chama cha TPLF kimetaja hatua hii ya kuondoka katika miji hii kama "mbinu ya kijeshi kwa kutaka kusonga mbele vizuri."

Wakati huo huo kiongozi wa kundi la Tigray People's Liberation Front (TPLF) nchini Ethiopia anasema vikosi vya Tigray vimeondoka katika maeneo ya Afar na Amhara.

Debretsion Gebremichael alisema hakutaka kutoa maelezo ya kwa nini vikosi vya Tigray vilijiondoa wakati walipokuwa wakikaribia mji mkuu Addis Ababa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.