Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Serikali ya Ethiopia yashutumu nchi za Magharibi kwa kuchochea vita

Nchini Ethiopia, vita vinaendelea kati ya serikali ya shirikisho na muungano wa waasi unaoongozwa na waasi wa Tigray. Kwa siku kadhaa sasa, vita vinaonekana vimesimama kwenye umbali wa takriban kilomita 200 kaskazini mwa mji mkuu Addis Ababa

Abiy Ahmed alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2019.
Abiy Ahmed alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 2019. Amanuel SILESHI AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abiy Ahmed amezuru mara mbili eneo lililo karibu na uwanja wa vita. Ushindi umekaribia, anasema. Kwa mara nyingine tena amewatolea wito waasi wa Tigraya kujisalimisha.

Baada ya balozi nyingi kutoa wito wa kuwarejesha makwao raia wao, serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ililalamikia msimamo wa balozi za nchi za Magharibi.

Inasikitisha sana kuona kwamba washirika wa kimkakati wanatumia kauli hii ya kutisha na mbaya. Tunafutlia mbali kabisa majaribio haya ya kuunda mazingira ya hofu na ukosefu wa usalama, amesema msemaji wake Billene Seyoum. Ni hotuba iliyokusudiwa kutimiza malengo ya kisiasa. 

Msemaji huyo anaenda mbali na kuyashutumu baadhi ya mataifa hayo ya kigeni kwa kuunga mkono kikamilifu waasi wa Tigray. Anahakikisha kwamba, kwa upande wa serikali, kila kitu kinafanyika ili kuzuia waasi wa tplf kusonga mbele.

Kipaumbele cha serikali ya Ethiopia ni kukomesha uhalifu unaofanywa na TPLF katika mikoa ya Afar na Amhara. Lakini hiyo haimaanishi kwamba mchakato wa amani hautafanyika. 

Mchakato huu wa amani unaongozwa na Umoja wa Afrika na mjumbe wake katika Pembe ya Afrika, rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo. "Ethiopia bado inaunga mkono juhudi hii kimsingi. Majadiliano ya amani ni jambo ambalo tumekuwa tukilitetea kila wakati ”, amebaini msemaji huyo.

Kwa mujibu wa wanadiplomasia na vyanzo kadhaa ndani ya Umoja wa Afrika, mchakato huu umekwama, huku pande zote mbili zikiamini kpata suluhu la mzozo huo kupitia vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.