Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Vikosi vya Ethiopia vyapunguza kasi ya kusonga mbele dhidi ya waasi wa Tigray

Raia wa kigeni wanaendelea kuondoka nchini Ethiopia. Jumamosi jioni Novemba 27, ndege ilikodishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ili kuwarudisha raia wa Ufaransa  jijini Paris.

Wanawake wakiwa wamesimama kando ya bango linaloonyesha Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed katika mkutano ulioandaliwa na maafisa wa Addis Ababa, unaoleta pamoja wasanii na wanariadha kuunga mkono mpango wa vita, tarehe 27 Novemba.
Wanawake wakiwa wamesimama kando ya bango linaloonyesha Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed katika mkutano ulioandaliwa na maafisa wa Addis Ababa, unaoleta pamoja wasanii na wanariadha kuunga mkono mpango wa vita, tarehe 27 Novemba. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Hatua hizi zinazochukuliwa na balozi nyingi ni kufuatia kusonga mbele kwa waasi wa Tigray, ambao kwa sasa kulingana na mashahidi wako kilomita 180 kaskazini mwa Addis Ababa. Lakini katika siku za hivi karibuni, jeshi la shirikisho linaonekana kupunguza kasi kusonga mbele dhidi ya waasi.

Katika kushawishi wananchi kujiunga na vikosi vya ulinzi kwenda vitani, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alitaka kuanzisha mashambulizi dhidi ya waasi. Na tangu wakati huo, vikosi vya shirikisho, vikisaidiwa na wanamgambo kutoka mikoa Afar na Amhara, vimeweza kuwazuia waasi kusonga mbele katika maeneo mbalimbali.

Kwanza mashariki katika eneo la Afar, ambapo jeshi la shirikisho na wanamgambo walichukua udhibiti wa miji miwili kutoka kwa waasi wa Tigray, huku wakitumia ndege zisizo na rubani, zilizonunuliwa hivi karibuni na Addis Ababa lakini ambazo walikuwa wamechelewa kuzitumia.

Katika eneo la Amhara, waasi wa Tigray wamekwama kwenye mlima wa Debre Sina, kilomita 180 kutoka Addis Ababa.

Wakati huo huo wito wa Waziri Mkuu kujiunga na vikosi vya ulinzi unaendelea kufanya kazi. Viongozi kadhaa wa kisiasa, kitamaduni na kimichezo wa Ethiopia wameunga mkono hadharani mpango wa kuungana na vikosi vya ulinzi katika vita dhidi ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.