Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Waziri Mkuu wa Ethiopia aingia kwenye mstari wa mbele wa vita dhidi ya waasi

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amekwenda kwenye uwanja wa vita kupambana moja kwa moja na waasi wa Tigray na washirika wake wanaodai wanateka miji kadhaa kuelekea jiji kuu Addis Ababa.

Siku ya Jumatatu, Abiy Ahmed ambaye pia ni mwanajeshi, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, wakati umefika wa yeye kwenda kwenye mstari wa mbele na kuongoza mapigano dhidi ya waasi wa Tigray.
Siku ya Jumatatu, Abiy Ahmed ambaye pia ni mwanajeshi, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, wakati umefika wa yeye kwenda kwenye mstari wa mbele na kuongoza mapigano dhidi ya waasi wa Tigray. © AP Photo/File
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Habari la serikali FANA, limeripoti kuwa Ahmed amekwenda katika mstari wa mbele kupambana na waasi, na kwa sasa madaraka nchini humo yanashikiliwa na naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen Hassen.

Msemaji wa serikali, Legesse Tulu katika mkutano na wanahabari, ameeleza kuwa baadhi ya majukumu ya serikali sasa yatatekelezwa na Naibu Waziri Mkuu.

Siku ya Jumatatu, Abiy Ahmed ambaye pia ni mwanajeshi, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, wakati umefika wa yeye kwenda kwenye mstari wa mbele na kuongoza mapigano dhidi ya waasi wa Tigray.

Wanariadha maarufu nchini hgumo, Haile Gebrselassie na  Feyisa Lilesa nao wamesema kuwa wako tayari kwenda kupambana baada ya tangazo la Waziri Mkuu Ahmed.  

Mwezi uliopita, waasi wa Tigray na washirika wake, walithishia kupambana mpaka jiji kuu Addis Ababa na wamekuwa wakifunga barabara ya kuelekea kwenye bandari ya Djibouti.

Kuendelea kwa mapambano ya kijeshi nchini Ethiopia, yanaathiri jitihada za kupata suluhu ya kisiasa kwa pande mbili, kwa mujibu wa mjumbe wa Marekani Jeffrey Feltman ambaye amekuwa  nchini Ethiopia.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha tangu mwezi Novemba mwaka uliopita, baaada ya kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi na waasi wa Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.