Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Serikali yaanza kuajiri wanajeshi wapya

Wakati muungano wa waasi unakaribia Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, serikali imeanza uaajiri wanajeshi wapya. Siku ya Jumatano, katika viunga vya mji mkuu, karibu vijana 1,200 walijiunga na vikosi vya ulinzi.

Mwanamume huyu akiwa ameshika bendera ya taifa la Ethiopia wakati wanajeshi wapya wanaojiunga na Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia wakihudhuria sherehe ya kuondoka mjini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Novemba 24, 2021.
Mwanamume huyu akiwa ameshika bendera ya taifa la Ethiopia wakati wanajeshi wapya wanaojiunga na Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia wakihudhuria sherehe ya kuondoka mjini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Novemba 24, 2021. © Amanuel Sileshi / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika wilaya ya Kolfe, vijana 18,000 kama Tewodros Tefera wamejiunga katika kundi la wanamgambo wa kujilinda. "Maisha hayana maana bila nchi thabiti. Ikiwa nitakufa kwenye uwanja wa vita, hali hii itawezesha familia yangu na vizazi vijavyo kuishi kwa uhuru na salama, " Tewodros Tefera amesema.

Lakini kwa sasa, Tewodros haendi vitani, anasubiri. Hata hivyo, angeweza kuitikia wito wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye alitangaza kwamba anataka kuongoza shughuli hizo yeye mwenyewe kutoka kwenye uwanja wa vita. "Tayari tunajua mifano ya Tewodros, Ménélik na Haile Selassie. Ni vivyo hivyo kwa Abiy Ahmed. Tunajua kwamba wakati kiongozi wako yuko mstari wa mbele na wewe, haurudi nyuma ”.

Baada ya siku chache za mafunzo katika eneo la kusini mwa Addis Ababa, vijana hao wanatarajia kuondoka kuelekea eneo la Amhara, ambako waasi wa Tigray wanaendelea kusonga mbele.

Hayo yanajiri wakati jana jumanne Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba utaziondoa ifikapo Novemba 25 familia za wafanyakazi wake wa kimataifa nchini Ethiopia, ambako mapigano yameendelea kuelekea mji mkuu, kulingana na waraka rasmi ulioandikwa Jumatatu ambao shirika la habari la AFP umepata kopi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.