Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USHIRIKIANO

Ufaransa yataka raia wake kuondoka Ethiopia 'bila kuchelewa'

Ufaransa imetoa wito kwa raia wake leo Jumanne kuondoka nchini Ethiopia "bila kuchelewa", ambako mapigano yanakaribia mji mkuu baada ya vita vya zaidi ya mwaka mmoja kati ya vikosi vya serikali na waasi kaskazini mwa nchi hiyo.

Hofu yatanda katika mji mkuu wa Ethiopia Addis-Ababa, baada ya waasi kusonga mbele kuelekea mji huo.
Hofu yatanda katika mji mkuu wa Ethiopia Addis-Ababa, baada ya waasi kusonga mbele kuelekea mji huo. © Wikimedia Commons/Mattias Kiel Nielsen
Matangazo ya kibiashara

"Raia wote wa Ufaransa wanaitwa rasmi kuondoka nchini bila kuchelewa," ubalozi wa Ufaransa mjini Addis Ababa umesema katika barua pepe iliyotumwa kwa wajumbe wa jamii ya Wafaransa waishio nchini Ethiopia.

Hayo yanajiri wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema sasa atawaongoza wanajeshi wake "kwenye uwanja wa vita."

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia, Abraham Belay, pia amebaini kwamba vikosi vya kijeshi hatimaye vitaanza "hatua tofauti", lakini bila maelezo zaidi. "Hatuwezi kuendelea hivi," amesema kwa urahisi.

Tangu Novemba mwaka jana, serikali na vikosi vya waasi vya Tigray People’s Liberation Front (TPLF) vimekuwa vikishiriki katika vita vilivyoanzia Tigray na kuenea katika mikoa jirani ya Amhara na Afar.

TPLF limeunda muungano na vikundi vingine vya waasi likiwemo Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA) huku mzozo huo ukikaribia mji mkuu.

Jeshi la Ethiopia likiwa limedhoofika sana, vita hivi sasa vinaendeshwa katika maeneo mbalimbali hasa na wanamgambo na vikosi vya majimbo. Na juhudi za kidiplomasia za Marekani na Umoja wa Afrika zinaonekana kukwama hivi leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.