Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ULINZI

Côte d’Ivoire kuongeza idadi ya wanajeshi wake

Akirejea Jumapili hii kutoka mjini Paris ambako alihudhuria Kongamano la Amani, rais Alassane Ouattara alitangaza kuajiri wanajeshi 3,000 mwaka ujao. Idadi ya wanajeshi inatarajiwa kuongezeka zaidi katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Hatua hiyo inakabiliana na changamoto za tishio la kigaidi ambalo linashadidi kutokana na mashambulizi kadhaa ya makundi yenye silaha kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Côte d’Ivoire wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Kijeshi cha Jacqueville karibu na Abidjan, Juni 10, 2021.
Wanajeshi wa Côte d’Ivoire wakati wa uzinduzi wa Chuo cha Kijeshi cha Jacqueville karibu na Abidjan, Juni 10, 2021. © REUTERS - Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Kuajiriwa kwa wanajeshi hawa 3,000 , zoezi lililopangwa katika bajeti ya 2022 ya Wizara ya Ulinzi,  kunaashiria wimbi la kwanza la uandikishaji wa vikosi vipya 10,000 kwa jumla vinavyotarajiwa kujumuisha jeshi la Côte d’Ivoire ifikapo 2024.

Tangazo la rais Alassane Ouattara linafuatia kikao cha Kamati ya wakuu wa majeshi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi, ECOWAS, wiki iliyopita mjini Abidjan. Majadiliano hayo yalihitimishwa juu ya hitaji la kugawana taarifa za kijasusi kati ya majimbo ya eneo hilo na uratibu wao wa hatua katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Tangu mwaka jana, Côte d'Ivoire imekuwa ikilengwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha katika ukanda wa Sahel, ambayo mara kwa mara yanafanya mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo, karibu na mpaka na Burkina Faso, ikiwa ni pamoja na ule wa Kafolo Juni mwaka jana ambapo wanajeshi kumi na wanne wa Côte d’Ivoire waliuawa.

Lakini uajiri huu pia utakuza ufufuaji wa nguvu kazi na kufidia wastaafu, kama kilivyobaini chanzo kimoja kutoka makao makuu ya jeshi kilielezea. Jeshi la Côte d’Ivoire lilikuwa maafisa wengi wakati kukiripotiwa uhaba wa askari. Uajiri hu unakuja kuweka sawa idadi inayohitajika kwa maafisa na wanajesi a ngazi ya chini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.