Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Sudan: Maandamano yasambaratishwa, watu kadhaa wauawa kwa risasi

Siku ya Jumatano Novemba 17, waandamanaji wasiopungua 15 walipigwa risasi na kufa wakati wa maandamano mjini Khartoum kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Jenerali al-Burhan. 

Wapinzani wamapinduzi katika mitaa ya Khartoum Kaskazini, Sudan, Novemba 13, 2021.
Wapinzani wamapinduzi katika mitaa ya Khartoum Kaskazini, Sudan, Novemba 13, 2021. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya hospitali vinavyounga mkono demokrasia, vimebaini kwamba watu kadhaa wamejeruhiwa, lakii wengi wamejeruhiwa vibaya. Hata hivyo vyombo vya usalama vimekanusha madai kuwa vilifyatua risasi za moto.

Ripoti ya hivi punde imebaini kwamba Jumatano ilikuwa siku mbaya zaidi tangu mapinduzi ya Oktoba 25. Katika Hospitali ya Royal Care, jioni, angalau vifo 15 vilirekodiwa, huku ikiongeza kuwa wengi walipigwa risasi. Hospitali ya Royal Care ilikuwa ikijiandaa kuwapokea wagonjwa kutoka wilaya ya Bourri.

Mzozo wa umwagaji damu kati ya raia na wanajeshi unaendelea. Chama cha Wataalamu wa Sudan kinashutumu polisi kwa "mauaji ya kukusudia". Kulingana na chama cha madaktari, waathiriwa wengi walipigwa risasi, huku vikosi vya usalama vikilenga "kichwa, kifua au shingo". Chama hicho kinawatuhumu wanajeshi wa Jenerali Burhan kwa kuwakimbiza waandamanaji hadi hospitalini na kuwarushia mabomu ya machozi watu waliojeruhiwa na magari ya wagonjwa.

Kwa mara nyingine tena, polisi, jeshi, vikosi vya usaidizi wa haraka na maafisa wa idara ya kijasusi wametumwa kwa wingi. Kwa lengo moja: kuzuia waandamanaji kwa nguvu zote.

Licha ya kukatwa kwa huduma ya simu katika vitongoji kadhaa, mikusanyiko ilifanyika. Pikipiki zilizunguka kutoka msafara mmoja hadi mwingine ili kuwahimiza waandamanaji ambao licha ya vikwazo vingi walivyokuwa wakikabiliana navyo siku nzima walijizatiti ili madai yao yasikike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.