Pata taarifa kuu
SENEGAL

Rais wa zamani wa Chad Hissene Habre kuzikwa nchini Senegal

Siku mbili baada ya kifo chake kutokana na gonjwa hatari la Covid-19 akiwa na umri wa miaka 79, Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré atazikwa Alhamisi hii Agosti 26 nchini Senegal.

Picha kutoka kwa kituo cha runinga cha Senegal wakati ikitaganzwa kesi ya Hissène Habré, Julai 20, 2015.
Picha kutoka kwa kituo cha runinga cha Senegal wakati ikitaganzwa kesi ya Hissène Habré, Julai 20, 2015. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu wakati suala la kurejeshwa kwa mwili wake nchini Chad lilipoibuka. Kiongozi huyo wa zamani wa Chad alikuwa akiishi nchini Senegal kwa miaka 31, baada ya kuondolewa mamlakani na Idriss Deby. Ni katika nchi hii ya Seneal ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2016 kwa uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa utawala wake kuanzia mwaka 1982 hadi 1990.

Mwili wa Hissène Habré imepangwa kupelekwa mapema Alhamisi alasiri, Agosti 26, katika msikiti wa Omar huko Dakar. Mazishi yatafanyika katika makaburi ya Waislamu ya Yoff katika mji mkuu wa Senegal.

► Soma pia: Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré aaga dunia

Kulikuwa na mvutano kati ya wake wawili wa Hissene Habre kuhusu wapi atazikwa mume wao, lakini pande zote mbili ziliafikiana na kuamua azikwe nchini Senegal.

Kwa sababu jioni siku alipofariki, Fatimé Raymonne Habré, mmoja wa wake zake, alitangaza kwamba anataka mumewe azikwe kwa muda "nchini Senegal" .

Itafahamika pia kwamba ni katika makaburi hayo ya Yoff ambapo alizikwa rais wa zamani wa Cameroon Ahmadou Ahidjo mwaka 1989. Alkimbilia uhamishoni nchini Senegal baada ya kuhukumiwa kifo akiwa hayupo nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.