Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Ethiopia: Muungano mpya wa kisiasa waundwa kuunga mkono waasi dhidi ya Abiy Ahmed

Mjumbe maalum wa Marekani Jeffrey Feltman ana kazi ngumu kutafuta suluhu na serikali kuhusu mkwamo wa kisiasa nchini humo, huku waasi ktoka makundi ya TPLF na Oromo wakikaribia mji mkuu wa Etiopia, Addis Ababa.

Wapiganaji wa TPLF huko Mekele, mji mkuu wa Tigray nchini Ethiopia, Julai 2021.
Wapiganaji wa TPLF huko Mekele, mji mkuu wa Tigray nchini Ethiopia, Julai 2021. Yasuyoshi Chiba AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Ni katika hali hii ya mvutano ambapo muungano mpya wa kisiasa umeundwa kuunga mkono waasi wa TPLF na Oromo, kwa kuonyesha kwamba vikosi mbalimbali vinaunga mkono upinzani wenye silaha dhidi ya serikali kuu ya Addis Ababa.

Waandalizi wake wameuita muungano huu mpya wa kisiasa na kijeshi Umoja wa Muungano wa Vikosi vya Shirikisho la Ethiopia. Unaundwa na makundi ya Tigray People's Liberation Front, TPLF, bila shaka, na Jeshi la Ukombozi la Oromo, OLA, makundi mawili ya kisiasa na kijeshi ambayo sasa yanaendesha vita dhidi ya vikosi vya shirikisho.

Wameungana na vuguvugu kutoka kwa watu walio wachache kama vile Benishangul, Agaw, Gambella, Kimant na Sidamas, na vyama kutoka majimbo yenye nguvu zaidi kama vile Wasomali na Waafar.

"Mkataba wa mpito nchini Ethiopia"

Mratibu wa muungano huu ameelezea vyombo vya habari kwamba unapaswa kutumika kupata "makubaliano ya mpito nchini Ethiopia" baada ya kuanguka kwa utawala wa Abiy Ahmed. Ni muungano kama huo,  chini ya mamlaka ya TPLF na Oromo, ambao ulimwangusha dikteta Mengistu mnamo 1991.

Kwa kujibu, msemaji wa serikali ya Ethiopia Billene Seyoum amesema tu kwamba "makundi hayo yaliyojitenga ambayo ymekataa mchakato wa kidemokrasia ulioanzishwa na Ethiopia mwaka wa 2018 hawawezi kukuza demokrasia leo."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.