Pata taarifa kuu
CONGO-BRAZZAVILLE

Congo-Brazzaville: Mwanasiasa wa upinzani Guy-Brice Parfait Kolélas aaga dunia

Mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini Congo-Brazzaville, Guy-Brice Parfait Kolélas, amefariki dunia siku chache baada ya kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 kabla tu ya mwishoni mwa juma hili lililopita.

Guy-Brice Parfait Kolélas amefariki Jumatatu Machi 22 kutokana na Corona.
Guy-Brice Parfait Kolélas amefariki Jumatatu Machi 22 kutokana na Corona. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Katika video iliyorushwa Jumamosi hii, Machi 20 ambapo alionekana dhaifu sana, alisema "alikuwa akipambana na kifo" na hata hivyo aliwataka wafuasi wake waende kupiga kura ili kuleta mabadiliko nchini Congo-Brazzaville.

 

Guy-Brice Parfait Kolélas amefariki dunia katika ndege iliyokuwa ikimpeleka nchini Ufaransa, ambako angepata matibabu. Mchumi huyu aliingia katika siasa akifuata nyayo za baba yake.

Kabla ya kuwa mmoja wa wapinzani wakuu wa Rais Sassou-Nguesso, Guy-Brice Parfait Kolélas baada ya kuhitimisha elimu yake katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Ufaransa, alifanya kazi katika Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Baba yake, Bernard Kolélas, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Pascal Lissouba.

Kolelas alivyopambana kisiasa na Sassou-Nguesso

Lakini wakati huo vita vya wenyewe kwa wenyewe viliibuka mnamo mwaka 1997, na Denis Sassou Nguesso akashinda vita hivyo. Bernard Kolélas na familia yake walilazimika kukimbilia nchini Mali.

Guy-Brice Parfait Kolélas mwenyewe alieleza hivi majuzi katika mkutano: "Baba yangu aliniomba niendelee na vita vya kisiasa. Aliniambia tu mimi, wala hakuwaambia wengine, wakati tulikuwa watoto 12 (wavulana na wasichana). "

Mapigano ya kisiasa ambayo yalimuweka kwenye nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016. Guy-Brice Parfait Kolélas alitaka kuona mabadiliko yakitokea nchini mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.