Pata taarifa kuu

Félix Tshisekedi akamilisha ziara yake Afrika Magharibi kwa kuzuru Guinea-Bissau

Rais wa DRC ambaye pia ni Rmwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika Félix Tshisekedi alianza ziara yake huko Afrika Magharibi Julai 15. Ziara yake ilianzia Ghana, Guinea na mwishowe Guinea-Bissau. 

Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi, Mei 18, 2021.
Rais wa DR Congo Félix Tshisekedi, Mei 18, 2021. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Hali nchini Mali, uhusiano mgumu kati ya rais wa Guinea Alpha Condé na mwenzake wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo vilijadiliwa katika mkutano wa marais Tshisekedi na Embalo.

Baada ya rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi, ambaye pia ni rais wa sasa wa Umoja wa Afrika, alizuru Guinea Bissau.

Ziara hiyo ni sehemu ya mfumo wa pande mbili, lakini hali nchini Mali ambapo rais Embalo anatamani kushiriki kibinafsi katika kutafuta suluhisho ilijadiliwa.

Pointi nyingine ya mshikamano iliyoijadiliwa katika mkutano wa marais hao wawili ni uhusiano tata kati ya rais wa Guinea Alpha Condé na mwenzake wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo. Kwa suala hili, rais Tshisekedi, ambaye alipokelewa huko Conakry siku ya Ijumaa, alisema kuwa hakuna shida kati ya nchi hizo mbili. "Sikujua walikuwa na shida," alisema rais wa DRC. Ni uhusiano ambao mtu anaweza kuwa nao kama kaka na mdogo wake. Guinea-Bissau na Guinea Conakry ni nchi mbili jirani na zenye udugu wa karibu, raia kutoka nchi hizi mbili ni ndugu na hilo ni muhimu kwangu, kinachosalia ni maelezo tu”.

Rais Embalo, kwa upande wake, amepuuzia mzozo huo, akisema kuwa hakuna mtafuru kati yake na kaka wake, Alpha Condé.

Mwezi Septemba mwaka jana, Rais Condé alichukua uamuzi wa kufunga mipaka ya nchi yake na majirani zake, Senegal, Guinea-Bissau na Sierra Leone. Hali hii ilizua vita vya maneno kati ya Marais Embalo na Condé katika mkutano wa 59 wa wakuu wa nchi huko Accra.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.