Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Majimbo 26 yatengwa katika duru ya pili ya uchaguzi kufuatia ukosefu wa usalama

Ethiopia imesema waaazi kutoka majimbo takribani 26 hawatoweza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi kutokana na kudorora kwa kiuslama katika majimbo hayo, wakati duru ya pili ya uchaguzi imepangwa kufanyika Septemba 30.

Katika duru ya kwanza ya mwezi Juni, Chama cha Waziri Mkuu Abiy Ahmed, Prosperity Party kiliweza kushinda muhula wa miaka mitano kwa kudai kushinda viti vya ubunge 410 kati ya viti 436 vya bunge la shirikisho.
Katika duru ya kwanza ya mwezi Juni, Chama cha Waziri Mkuu Abiy Ahmed, Prosperity Party kiliweza kushinda muhula wa miaka mitano kwa kudai kushinda viti vya ubunge 410 kati ya viti 436 vya bunge la shirikisho. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa bodi ya uchaguzi, Solyana Shimeles amesema kuwa duru ya pili ya uchaguzi haitofayika katika majimbo 18 ya eneo la Amhara na manane ya Oromia, huku akiongeza kuwa hawajaamua kwa jinsi gani na lini uchaguzi utafanyika katika maeneo haya.

Mapigano bado yanaripotiwa katika eneo la Amhara kati ya majeshi ya serikali na kundi la wapiganaji wa chama cha ukombozi wa watu wa Tigray, TPLF, wakati Oromia inapambana na uasi wa Jeshi la Ukombozi la Oromo OLA.

Uchaguzi huo pia hautafanyika katika baadhi ya majimbo kama ya Afar na Benishangul-Gumuz, bodi hiyo ilisema, ingawa haikutoa ufafanuzi wa idadi ya maeneo yanayolengwa.

Bii. Solyana amesema matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Septemba 30 yatatangazwa Oktoba 10.

Katika duru ya kwanza ya mwezi Juni, Chama cha Waziri Mkuu Abiy Ahmed, Prosperity Party kiliweza kushinda muhula wa miaka mitano kwa kudai kushinda viti vya ubunge 410 kati ya viti 436 vya bunge la shirikisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.