Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA

Guinea: Mamady Doumbouya kutawazwa Ijumaa hii

Luteni-Kanali Mamady Doumbouya anatarajia kuwa rasmi rais wa Jamhuri ya Guinea Ijumaa hii, Oktoba 1. Kiongozi huyu mkuu wa mapinduzi ambaye alimpindua Alpha Condé mwezi mmoja uliopita ataapishwa huko Conakry mbele ya Mahakama Kuu Ijumaa hii Oktoba 1, 2021.

Kanali Doumbouya amezungukwa na wajumbe wa CRND. Septemba 17, 2021.
Kanali Doumbouya amezungukwa na wajumbe wa CRND. Septemba 17, 2021. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Wanadiplomasia wa kigeni waliopo nchini, pamoja na wakuu wa nchi, wamealikwa kuhudhuria hafla hiyo. Lakini wakati Kamati ya Taifa kwa ajili ya Maendeleo ya Guinea, CNRD, bado inakabiliwa na vikwazo vya Jumuyia ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, swali linaibuka kuhusu uwepo wa wageni hawa kwenye sherehe ya kuapishwa kwa rais Mamady Doumbouya.

Pamoja na siku hii kutangazwa likizo kwa wafanyakazi wa serikali na wake katika sekta binafsi, ni Guinea itakuwa katika kipindi cha siku mbili katika sherehe mbalimbali. Kwa sababu Luteni-Kanali Mamady Doumbouya amechagua kula kiapo kabla tu ya sikukuu ya kitaifa itakayofanyika Jumamosi hii. Kwa hivyo ni baada ya kuapishwa na kuwa rais wa mpito ambapo atasherehekea maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Guinea.

Sherehe ya kutawazwa itafanyika katika ukumbi wa Mohamed V mbele ya majaji wa Mahakama Kuu, sherehe ambayo itaanza saa sita mchana.

Chanzo kilicho karibu na waandaaji wa hafla hiyo kinasema majenerali wa jeshi, wanasiasa, na wafanyabiashara watahudhuria sherehe hiyo. Mialiko ilitumwa kwa mabalozi wa mataifa ya kigeni nchini Guinea. Kwa wakati huu, bado haijulikani ni viongozi wangapi kutoka nch za kigeni watahudhuria sherehe hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.