Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE

Côte d’Ivoire yaomboleza kifo cha waziri wa zamani Charles Konan Banny

Wanasiasa mbalimbali na wanaharakati nchini Côte d’Ivoire wanaendelea kutoa rambi rambi zao, tangu Ijumaa, Septemba 10 baada ya kutangazwa kifo cha Charles Konan Banny, aliyefariki dunia nchini Ufaransa, akiwa na umri wa miaka 78.

Charles Konan Banny, Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire, alifariki jijini Paris, Ufaransa, akiwa na umri wa miaka 78,  Septemba 10, 2021.
Charles Konan Banny, Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire, alifariki jijini Paris, Ufaransa, akiwa na umri wa miaka 78, Septemba 10, 2021. AFP Photo / Sia Kambou
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Benki kuu ya mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO) kwa miaka kumi na tano, Charles Konan Banny alihudumu kama waziri mkuu wa Chad kwa kipindi cha miezi kumi na sita, kati ya mwaka 2005 na 2007. Pia aliongoza Tume ya Mazungumzo, Ukweli na Maridhiano (CDVR) kuanzia mwaka 2011 hadi 2014.

Charles Konan Banny alijulikana kuwa mtu wa asiyejifaharisha, ambaye alikuwa na uhusiano mzuri na wanasiasa karibu wote.

"Charles Konan Banny alikuwa mtumishi mkubwa wa Serikali, mtu mashuhuri wa kisiasa ambaye mchango wake katika upatanisho wa kitaifa ulikuwa muhimu", amesema kwenye mitandao ya kijamii rais Alassane Ouattara, saa machache baada ya kifo cha mrithi wake mkuu wa Benki Kuu ya mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.