Pata taarifa kuu

WHO yatangaza kumalizika mlipuko wa pili wa Ebola nchini Guinea

Shirika la Afya Ulimwenguni Jumamosi iliyopita lilitangaza rasmi kumalizika kwa wimbi la pili la ugonjwa wa Ebola nchini Guinea ambao ulitangazwa mwezi Februari kuwaua watu 12.

Timu ya manensi wakitoa chanjo dhidi ya Ebola katika hospitali ya N’Zérékoré nchini Guinea February 24 2021.
Timu ya manensi wakitoa chanjo dhidi ya Ebola katika hospitali ya N’Zérékoré nchini Guinea February 24 2021. © AFP - Carol Valade
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya kesi 16 za wagonjwa wa Ebola kuthibitishwa ambapo saba zinaendelea kufanyiwa uchunguzi wakati huu kukiwa na kupungua kwa idadi ya wagoinjwa, ripoti ya shirika la afya ulimwenguni WHO, imefahamisha.

Shirika hili limetangaza kumalizika rasmi kwa Ebola huko Guinea ikiwa miezi minne imepita tangu WHO litangaze kutuma chanjo 11,000 za ebola nchini humo ili taifa hilo liweze kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ulilotangazwa katika eneo la Kusini la N'Zerekore.

Umoja wa Mataifa kwa upande wake ulitangaza kutoa msaada wa fedha wa dola milioni 15 kutoka katika mfuko wake wa dharura ili kuisaidia Guinea na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kupambana na janga hilo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mwanzoni mwa mwezi mei ugonjwa ambao ulioripotiwa hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu sita na wengine 12 kuambukizwa mkoani Kivu Kaskazini

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.