Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-AFYA

Mgonjwa wa virusi vya Ebola Cote d'Ivoire apona

Msichana kutoka Guinea aliyegunduliwa na virusi vya Ebola nchini Cote d'Ivoire amepona. Msichana huyo aliwasili chini  Cote d'Ivoire Agosti 11 akitokea nchini Guinea, wizara ya afya ya Cote d'Ivoire iilisema Jumanne wiki hii.

DAbiria wakifanyiwa vipimo, kama sehemu ya mapambano dhidi ya Ebola, huko Abidjan, Juni 13, 2014.
DAbiria wakifanyiwa vipimo, kama sehemu ya mapambano dhidi ya Ebola, huko Abidjan, Juni 13, 2014. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

"Tulimfanyia mgonjwa vipimo viwili vya kibaolojia ambapo alikutwa hana tena virusi vya Ebola ndani ya saa 48. Kwa hivyo msichana huyo amepona" , ameliambia shirika la habai la AFP Serge Eholié, msemaji wa Wizara ya Afya na mkuu wa idara ya magonjwa ya kuambukiza kati Treichville Hospitali ya Chuo Kikuu huko Abidjan, ambayo ilikuwa ikimhudumia kimatibabu mgonjwa.

"Kuanzia sasa (Jumanne) mwanamke huyo hataendelea kuwekwa karantini. Bado amechoka, ataendelea kubaki hospitalini" ameongeza Profesa Eholié.

"Kuanzia leo (Jumanne) tunahesabu siku 42 kuweza kusema ikiwa Côte d'Ivoire haina tena kisa chochote cha maambukizi ya Ebola," amebaini.

Agosti 14 mamlaka ya afya nchini Cote d'Ivoire iligundua kesi ya Ebola kwa msichana wa miaka 18 wa Guinea, aliyewasili Cote d'Ivoire Agosti 11 kutoka mji wa Labine (kaskazini) mwa Guinea.

Ugunduzi huu ulikuwa kesi ya kwanza kuthibitishwa nchini Cote d'Ivoire tangu mwaka 1994, katika nchi hii jirani na Guinea iliyoathiriwa sana na ugonjwa huo kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2016 na ambapo virusi hivyo viligunduliwa tena mnamo mwaka 2021.

Visa arobaini na tisa vya watu ambao walitangamana na msichana huyo kutoka Guinea wametambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Cote d'Ivoire ni nchi ya tatu katika bara la Afrika mwaka huu kuathiriwa na virusi vya Ebola baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Guinea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.