Pata taarifa kuu
GUINEA

Guinea: Mvutano waibuka baada ya mwanasiasa wa upinzani kufariki gerezani Conakry

Mooja wa wanasiasa wa upinzania aliyekuwa akizuiliwa nchini Guinea tangu mwezi Septemba katika jela katika mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry, alifariki dunia usiku wa Jumatano 16 kuamkia Alhamisi Desemba 17.

Rais wa Guinea, Alpha Conde.
Rais wa Guinea, Alpha Conde. REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Roger Bamba, aliyekuwa na umri wa miaka arobaini, alikuwa afisa wa mawasiliano na kiongozi wa kundi la vijana katika chama cha UFDG, chama kikuu cha upinzani, kinachoongozwa na Cellou Dalein Diallo.

 

Alikufa saa chache baada ya kupelekwa hospitali katika mji mkuu Conakry. Alikamatwa baada ya kupeana ujumbe kuhusu ya hali ya kisiasa nchini, kulingana na mkewe, ambaye anashutumu mamlaka kwa unyanyasaji na uhalifu uliotekelezwa na maafisa wa serikali.

 

Diabaty Doré, kiongozi wa chama cha upinzani cha RPR na mwanachama wa muungano uliomuunga mkono Cellou Dalein Diallo wakati wa uchaguzi wa rais, ambaye alikuwa karibu na Roger Bamba amelaani mazingira ambamo mwanasiasa huyo alikuwa akizuiliwa.

 

"Nimemkosa rafiki na mtetezi wa demokrasia, " amesema Diabaty Doré.

 

"Alikuwa akizuiliwa katika chumba kinachopima ukubwa wa 7m² na walikuwa watu tisa katika chumba hicho. Pamoja na watu tisa, walikuwa wakilalaje? Haya ni mazingira mabaya sana katika nchi kama hii ya Guinea. Na tunalaumiwa nini? Hakuna anayejua ! Alikamatwa kwa sababu tu ya maoni yake! " ameongeza Diabaty Doré.

 

 Kifo cha Roger Bamba gerezani, kimetokana na ukosefu wa huduma, familia yake imepoteza, na chama cha UFDG pia kimepoteza kiungo miuhimu, Cellou Dalein Diallo ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

 

Hata hivyo msemaji wa Wizara ya Sheria, Sékou Keita, hajazungumzoa chochote kuhusiana na madai hayo ya upinzani. Lakini amehakikisha kwamba utaratibu wa kisheria uliheshimiwa, na kubaini kwamba Roger Bamba alifariki dunia kwa ugonjwa wa ini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.