Pata taarifa kuu
CONGO-BRAZZAVILLE

Congo-Brazzaville: Sassou-Nguesso aibuka mshindi kwa 88.57% ya kura

Rais wa Congo-Brazzaville anayemaliza muda wake , Denis Sassou-Nguesso, amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo kwa 88.57% ya kura kwa kipindi cha miaka mitano, kulingana na matokeo rasmi ya awali ya Tume ya Uchaguzi, yaliyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani.

Mkutano wa wafuasi wa Denis Sassou Nguesso, mgombea wa urais anayemaliza muda wake, Brazzaville  Machi 19, 2021..
Mkutano wa wafuasi wa Denis Sassou Nguesso, mgombea wa urais anayemaliza muda wake, Brazzaville Machi 19, 2021.. © REUTERS/Hereward Holland
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Ndani, Raymond Mboulou, Jumanne hii alasiri amesoma matokeo kutoka wilaya kwa wilaya moja kwa moja kwenye runinga ya serikali. Saa mbili za kutangazwa kwa matokeo ambayo yalikuwa mkusanyiko wa ushindi kwa rais anayemaliza muda wake, ambaye kwa upande wake takwimu za tume ya uchaguzi zinatoa ushindi mkubwa.

Denis Sassou-Nguesso, mwenye umri wa miaka 77, pamoja na miaka 37 akiwa madarakani kama rais wa nchi, ameshinda kila maeneo. Katika ngqzi ya kitaifa, tume ya uchaguzi inampa ushindi wa 88.57% ya kura, ambayo ni zaidi ya kura 700,000 za ziada ikilinganishwa na mwaka 2016, wakati alipopata 60.19% ya kura.

Upinzani kuwasilisha malalamiko yao mbele ya mahakama ya Katiba

Miongoni mwa wagombea wengine sita katika kinyang'anyiro hicho, ni Guy-Brice Parfait Kolélas aliyefariki Jumapili jioni kwa ugonjwa wa COVID-19 mara tu baada ya kuwasili nchini Ufaransa ambaye anahesabiwa kuwa na kura nyingi, baada ya kupata 7.84%. Waziri wa zamani Mathias Dzon amepata 1.90% ya kura na wagombea wengine wako chini ya 1%  ya kura. Kiwango rasmi cha ushiriki kilifikia 67.55%.

Wapinzani tayari wametangaza kwamba watawasilisha malalamiko yao mbele ya mahakama ya Katiba, Washirika wa karibu wa Guy-Brice Parfait Kolélas wamelaani udanganyifu mkubwa wa kura. Mathias Dzon, kwa upande wake, almebaini kwamba "uchaguzi huo haueleweki". Sasa wana siku tatu kuwasilisha malalamiko yao kwa mahakama ya katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.