Pata taarifa kuu
CHAD

Chad haifikirii kuandaa mazishi ya Hissene Habre

Serikali ya Chad inasema haina mpango wa kuandaa mazishi ya kitaifa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hissene Habre, aliyefariki dunia siku ya Jumanne baada ya kuambikizwa virusi vya Corona, akiwa na umri wa miaka 79.

Dikteta wa zamani wa Chad Hissene Habre, akisindikizwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa na jaji, Julai 2, 2013 huko Dakar.
Dikteta wa zamani wa Chad Hissene Habre, akisindikizwa na wanajeshi baada ya kusikilizwa na jaji, Julai 2, 2013 huko Dakar. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Dikteta huyo wa zamani alikuwa anatumikia kifungo cha maisha jela jijini Dakar nchini Senegal kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu wakati alipokuwa madarakani kati ya mwaka 1982 mpaja 1990.

Hata hivyo, Abderaman Koulamallah Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya Chad anasema hakuna kizuizi cha mwili wa kiongozi huyo wa zamani kurejeshwa nyumbani kuzikwa.

Uvumi wa kifo cha rais wa zamani wa Chad ulianza jioni ya Jumatatu, Agosti 23 na taarifa kutoka kwa mke wa Hissène Habré, Fatimé Raymonne Habre, ambaye alibaini kuwa rais huyo wa zamani alikuwa ameambukizwa virusi vya Covid-19. Lakini kwa upande wake, mamlaka ya magereza nchini Senegal ilisema kwamba hakuna kesi ya Covid-19 iliyorekodiwa katika jela alikokuwa amezuiliwa, ameripoti mwandishi wetu huko Dakar, Théa Olivier.

Kwa hivyo aliambukizwa wakati alipokuwa katika kliniki ya kibinafsi kabla ya kutibiwa katika hospitali ya umma, kulingana na mkewe. Habari ambayo imethibitishwa na Waziri wa Sheria wa Senegal.

Hissène Habré alikuwa kizuizini "huko Cap Manuel, siku chache zilizopita," Waziri Malick Sall ameiambia RFI. Mkewe ndiye ambaye alizungumza kuhusu hali yake ya afya: "Kwa hivyo aliomba ahamishwe kwa kliniki ya daraja la kwanza huko Dakar," ameongeza Waziri Malick Sall.

Habre ambaye serikali yake ilituhumiwa kwa mauaji ya maelfu ya watu na kuwa kiongozi wa kwanza wa nchi kuhukumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na mahakama ya Afrika baada ya kuishi uhamishoni Senegal kwa miongo mingi alifariki katika hospitali moja ya mjini Dakar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.