Pata taarifa kuu
CHAD-USHIRIKIANO

Je hatua ya Chad itaathiri kijeshi kikosi cha G5 Sahel?

Wengi wanahoji hatua ya Chad kuondoa askari wake 600 waliotumwa kama sehemu ya kikosi cha kikanda cha G5 Sahel ikiwa itaathiri hatua za kijeshi katika uwanja wa mapambano? Jeshi la Ufaransa limehakikisha kuwa kikosi cha G5 kitaendelea kufanya operesheni zake kama ilivyo kuwa.

Wanajeshi wa Chad wakiwa na magari ya kijeshi wakati wa sherehe huko Ndjamena, Januari 2021.
Wanajeshi wa Chad wakiwa na magari ya kijeshi wakati wa sherehe huko Ndjamena, Januari 2021. AFP - RENAUD MASBEYE BOYBEYE
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kuondolewa kwa wanajeshi 600 kati ya 1,200 waliopelekwa kama sehemu ya kikosi cha kikanda cha G5 Sahel linakuja wakati mashambulio ya wanajihadi yanaongezeka katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu" na wakati jeshi la Ufaransa lilitangaza kumalizika kwa Operesheni Barkhane na limeanza kupunguza idadi ya wanajeshi wake.

Kwa mujibu wa msemaji wa makao makuu ya jeshi la Ufaransa, Kanali Pascal Lanni, kikosi hiki kilikuwa hakizoei hali ilivyo katika uwanja wa mapambano. “Kikosi hiki cha wanajeshi 1,200, kilipopelekwa, kilikuwa na vifaa vya kutosha, magari ya kivita na silaha kubwa za kivita. Lakini hakikufanya vema katika eneo la  mipaka mitatu. "

"Unapopeleka kitengo cha wanajeshi waliozoea kutumia silaha kubwa silaha kwa magari ya kijeshi," Kanali Ianni ameongeza, "huwezi kukibadilisha kuwa kitengo cha wanajeshi wa ardhini wanaotembea kwa mguu kwa urahisi. "

"Chad inaendelea kujitolea sana katika vikosi vya G5 Sahel"

Kupungua kwa idadi ya vikosi vya Chad kunakuja siku chache baada ya kutangazwa kumalizika kwa operesheni Barkhane na kupungua kwa idadi ya wanajeshi wa Ufaransa ambao angelishirikiana na vikosi vya G5 Sahel.

Kwetu, hii sio habari mbaya, ni uamuzi huru uliochukuliwa na serikali ya Chad kwa kushirikiana na nchi za G5 Sahel. Chad inaendelea kujitolea katika vikosi ya G5 Sahel. 
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.