Chad yawarejeha nyumbani wanajeshi 600 kutoka kikosi cha G5 Sahel
Chad imetangaza kwamba imeondoa nusu ya wanajeshi wake waliopelekwa mwezi Februari katika kikosi cha kupambana na wajihadi cha G5 Sahel katika eneo linaloitwa "mipaka mitatu", maeneo ya mpaka wa Mali, Niger na Burkina Faso.
Imechapishwa:
Msemaji wa serikali ya Chad Abderaman Koulamallah, amesema idai hiyo haitzuia jitihada ya kikosi hicho kupambana na wanajihadi.
Kikosi hicho kilifika siku ya Alhamisi jioni katika nchini Chad baada ya zoezi la kuondoka lililoratibiwa na washirika wa G5 Sahel na Ufaransa vyanzo vya usalama kutoka Chad vimebaini.
Wanajeshi hao ni 600, nvimebaini vyanzo hivyo, ambavyo vimeongeza kuwa maelfu ya waasi wamekuwa wakitafuta kwa miezi kadhaa kurudi katika mji mkuu.
Kwa hivyo ni mbinu ya mkakati ambayo haitabadilisha chochote katika vita dhidi ya ugaidi huko Sahel, amesema msemaji wa serikali ya Chad, Abdéramane Koullamallah.