Pata taarifa kuu
SUDAN-HAKI

Sudan yachukua hatua nyingine kuelekea kumkabidhi Omar al-Bashir ICC

Sudan itamkabidhi Omar El-Bashir kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai,ICC. Tangazo hilo limetolewa Jumatano Agosti 11 na Waziri wa Mambo ya nje, siku ya pili ya ziara ya mwendesha mashtaka mpya wa ICC, Karim Khan, jijini Khartoum, nchini Sudan.

Omar al-Bashir katika mahakama ya Khartoum Agosti 2019.
Omar al-Bashir katika mahakama ya Khartoum Agosti 2019. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Sudan kwa miaka mingi amekuwa chini ya waranti mbili za kimataifa za kukamatwa zilizotolewa na ICC kwa uhalifu dhidi ya binadam na mauaji ya halaiki huko Darfur.

Katika miezi ya hivi karibuni, mamlaka ya Sudan ilikuwa imeongeza ishara za ushirikiano na Mahakama hyo ya kimataifa. Leo, ni Baraza la Mawaziri ambalo limefanya uamuzi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Mariam al-Mahdi, ametangaza hili wakati wa mkutano na mwendesha mashtaka wa ICC. Ni viongozi wa tatu wa zamani wa Sudan wanaotuhumiwa uhalifu huko Darfur ambao wanapaswa kukabidhiwa kwa ICC: Rais wa zamani Omar al-Bashir, lakini pia Ahmed Haroun, gavana wa zamani wa Jimbo la Kordofan Kusini, na Abdel Rahim Mohamed Hussein, Waziri wa zamani ya Ulinzi. Inabakia kujua wakati na katika mazingira gani zoezi hilo litafanyika.

Wiki iliyopita, baraza la mawaziri la Sudan lilikuwa tayari limechukua hatua kuelekea ushirikiano mkubwa na Mahakama ya kimataifa huko Hague kwa kutangaza kwamba ilikuwa imepitisha muswada unaolenga kuridhia Mkataba wa Roma wa ICC.

"Haki kwa uhalifu uliofanywa Darfur"

Baada ya mapinduzi ya Sudan, mamlaka ya mpito ilijapa kumfikisha Omar El-Bashir mbele ya ICC. Lakini hadi sasa, alikuwa bado ameshikiliwa Khartoum, katika gereza la Kober, akihukumiwa kwa ufisadi na kushtakiwa katika kesi nyingine inayohusiana na mapinduzi yaliyomwingiza mamlakani mwaka 1989.

Hakuna majibu kutoka ICC kwa sasa. Lakini "haki kwa uhalifu uliofanywa Darfur" lilikuwa lengo kuu la ICC, kwa maneno ya mwendesha mashtaka wa zamani Fatou Bensouda alipozuru Sudan miezi michache iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.