Pata taarifa kuu
SUDAN-HAKI

Bensouda ataka washukiwa wa uhalifu wa kivita Darfur kufikishwa ICC

Kiongozi wa Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC Fatou Bensouda ambaye amekuwa ziarani nchini Sudan, ametoa wito kwa serikali nchini humo kusaidia kumfikisha Ahmed Haroun katika Mahakama hiyo kujibu mashtaka ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur.

Mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda azungumza na waandishi wa habari huko Nyala Kusini mwa Darfur Mei 31, 2021.
Mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda azungumza na waandishi wa habari huko Nyala Kusini mwa Darfur Mei 31, 2021. AFP - ABDELMONIEM MADIBO
Matangazo ya kibiashara

Haroun, ni miongoni mwa washukiwa wanaotakiwa na ICC pamoja na rais wa zamani Omar al-Bashir na kiongozi wa kundi la Janjaweed  Abd-Al-Rahman ambaye alijiwasilisha kwenye Mahakama hiyo mwaka uliopita.

Bensuda anasema ana uhakika majaji wa Mahakam aya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, watathibitisha mashtaka dhidi ya Ahmed Haroun. 

Ukianza na mfano wa Ahmed Haroun, ambaye nilchukua muda kuelezea kuwa majaji wanaosikiliza kesi ya kuthibitisha mashtaka, wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kufikia mwisho wa mwezi wa Julai, kuamua iwapo mashtaka yatathitibitishwa au la.………Tuna uhakika kuwa kwa namna tumewasilisha kesi yetu, tunaamini kuwa mashataka hayo yatathibitishwa.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.