Pata taarifa kuu
SUDANI-ICC-HAKI

Ali Kushayb kufikishwa mbele ya Mahakama ya ICC

Kiongozi wa wanamgambo wa Janjawidi, Ali Kushayb, anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC kujjibu tuhuma zinazomkabili. Anatuhumiwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur, nchini Sudan.

Mahakama makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, huko Hague. (picha ya kumbukumbu)
Mahakama makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, huko Hague. (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Jerry Lampen
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyu wa wanamgambo wa kundi la Janjawidi amekuwa akisakwa na Mahakama ya Kimataifa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kwa kipindi chote cha karibu miaka 15.

Alivuka mpaka wa Sudan mapema mwaka huu kwenda Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ali Kushayb alikamatwa baada ya mchakato wa miezi kadhaa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kulingana na vyanzo kadhaa vya kuaminika, Ali Kushayb aliishi kwa kipindi cha miezi kadhaa katika jiji la Birao na familia ya watu mashuhuri mwanzoni mwa mwaka huu, kabla ya kuondoka kwenda mafichoni. Lakini kulikuepo na mawasiliano na mshtumiwa huyo ambayo alitaka kwa muda mrefu kujisalimisha mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.

Ilichukua muda hasa kujua ni Ali Kushayb, ambaye alikuwa akitafutwa na ICC. Siku ya Jumapili wiki moja iliyopita, Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eric Didier Tambo kwa msaada wa ICC na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINISCA, hasa alikwenda katika mji wa Birao ili kuweza kumkamata.

Ali Kushayb, kiongozi wa wanamgambo wa kundi la Janjawidi, mwenye umri wa karibu miaka 70, alimfahamisha mwendesha mashtaka kwamba anapendelea kushitakiwa na ICC badala ya nchini Sudani akihofia kwamba hatatendewa haki.

Baada ya kujisalimisha huloi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Fatou Bensouda amekaribisha "hatua yenye maamuzi" ili haki itendeke kwa waathiriwa wa vita huko Darfur.

Katika hotuba yake fupi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano wiki iliyopita, Fatou Bensouda alisema kuwa ana "matumaini" kuhusu hatma ya Sudan katika siku za hivi karibuni na kutoa wito kwa serikali ya Khartoum kufanya "mazungumzo", hata kama hatma ya washtakiwa wengine wa Sudani waliyohukumiwa na ICC bado haijajulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.