Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Raia wa Ethiopia wasubiri matokeo baada ya kupiga kura siku ya Jumatatu

Raia wa Ethiopia wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika siku ya Jumatatu, katika nchi hiyo ya pembe ya Afrika inayoshuhudia mzozo na ukame katika jimbo la Kaskazini la Tigray, uchaguzi ambao Waziri Mkuu Abiy Ahmed amesema utadhihirisha ukomavu wa demokrasia nchini humo.

Wananchi wa Ethiopîa wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu
Wananchi wa Ethiopîa wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu Eduardo Soteras AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu ni kama kipimo cha demokrasia katika nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, inayooongozwa na Waziri Ahmed ambaye wadadisi wa siasa wanaona kuwa chama chake cha Prosperity Party kilichokuwa na wagombea wengi, kinatarajiwa kushinda.

Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki na kinachoendelea kwa sasa ni zoezi la kuhesabu kura, na matokeo yanatarajiwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi baada ya siku kadhaa.

Hata hivyo, wakaazi wa jimbo lenye mzozo la Tigray na maeneo maeneo yenye changamoto za usalama hawakupiga kura, na sasa watawachagua wawakilishi wao tarehe sita mwezi septemba.

Vyama vya upinzani vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huu kikiongozwa na kile cha Ethiopian Citizens for Social Justice, vimedai kuwepo kwa udanganyifu kwenye kwa madai kuwa mawakala wao wametishwa na kuhitilafiwa kwa masanduku ya kuhifadhi kura.

Wapiga kura Milioni 38 waliruhusiwa kushiriki kwenue uchaguzi huo kuwachagua wabunge kati ya wagombea zaidia ya Elfu Tisa walionawania katiika majimbo mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.