Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Waziri Mkuu Abiy Ahmed: Jeshi la Eritrea litaondoka Tigray

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Ali ametangaza leo Ijumaa Machi 26 kuwa Eritrea itaondoa wanajeshi wake kutoka mkoa wa Tigray (kaskazini mwa Ethiopia), ambapo Addis Ababa ilianzisha operesheni ya kijeshi mnamo mwezi wa Novemba 2020 kuwaondoa mamlakani viongozi walioasi.

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed. REUTERS/Kumera Gemechu
Matangazo ya kibiashara

"Katika mazungumzo yangu ya Machi 26 na Rais wa (Eritrea) Issaias Afeworki wakati wa ziara yangu huko Asmara, serikali ya Eritrea ilikubali kuondoa vikosi vyake nje ya mipaka ya Ethiopia," waziri mkuu amesema katika taarifa, iliyorushwa kwenye ukurasa wake wa Twitter iliyonukuliwa na AFP.

Tangazo hilo linafuatia na kauli ya waziri huyo mkuu kukiri Jumanne wiki hii, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi huko Tigray, uwepo wa wanajeshi wa Eritrea katika jimbo laTigray.

Abiy AHmed alizuru Asmara siku ya Alhamisi wiki hii.

Operesheni ya Addis-Ababa dhidi hya TPLF

Waziri Mkuu wa Ethiopia alizindua operesheni ya kijeshi Novemba 4, 2021 iliolenga kukiondoa mamlakani chama tawala kaskazini mwa nchi, Tigray People's Liberation Front (TPLF), ambaye alivituhumu vikosi vyake kushambulia kambi za jeshi la shirikisho.

Alitangaza ushindi mnamo Novemba 28, lakini mapigano yaliendelea .

Katika taarifa yake leo Ijumaa, amekumbusha kwamba TPLF ilirusha roketi kadhaa katika mji mkuu wa Eritrea, "na hivyo kusababisha serikali ya Eritrea kuvuka mpaka na kuingia Ethiopia, kuzuia mashambulio zaidi na kulinda usalama taifa lake".

Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya 2019 ameongeza kuwa jeshi la Ethiopia litatumwa katika maeneo ambayo askari wa Eritrea walikuwa wakipiga kambi, hasa kwenye mpaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.