Pata taarifa kuu
SUDANI-ICC-HAKI

ICC yatoa wito kwa washukiwa wa uhalifu wa kivita Sudan kujisalimisha

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ya ICC, inawataka washukiwa inayowatafuta kutoka nchini Sudan kujisalimisha haraka iwezekanavyo, kabla hawajakamatwa na vyombo husika na kupelekwa Hague, makao makuu ya mahakama hiyo ya kimataifa.

Jengo la Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi
Jengo la Mahakama ya Kimataifa ya ICC mjini Hague nchini Uholanzi © ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja siku moja baada ya mshukiwa mmoja Ali Kushayb kujisalimisha katika Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Hague nchini Uholanzi.

Kujisalimisha huko kumethibitshwa na kiongozi wa Mashtaka Fatou Bensouda na kusema mshukiwa huyo anayetuhumiwa kutekelza makosa ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur, amejisalilimisha nchini Jalmhuri ya Afrika ya Kati.

Rais wa zamani Omar Al Bashir anatafutwa na Mahakama hiyo.

Mapema mwaka huu serikali ya Sudan na makundi ya waasi katika jimbo tete la Darfur walikubaliana katika mazungumzo ya amani mjini Juba juu ya kuwafikisha mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC Omar al Bashir na wenzake wanaotafutwa na mahakama hiyo.

Bashir ambaye aliondolewa madarakani na jeshi mwaka jana kutokana na maandamano ya umma, anasakwa na ICC kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu na mauaji ya halaiki yanayohusiana na mgogoro wa Darfur. Tangu kuangushwa kwake Aprili, amekuwa kizuizini mjini Khartoum, kwa mashitaka ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji.

Mahakama ya The Hague ICC imemfungulia mashtaka kiongozi huyo wa zamani wa Sudan pamoja na wasaidizi wake wa zamani watatu kwa makosa ya mauaji ya halaiki,uhalifu dhidi ya ubinadamu na na uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur kufuatia mgogoro wa kikatili uliozuka mwaka 2003. Uamuzi huo umefikiwa Juba katika mazungumzo yaliyolenga juu ya kutafutwa  haki na maridhiano katika jimbo la Darfur.Takriban watu 300,000 waliuwawa  na mamilioni ya wengine waliachwa bila makaazi ulipozuka mgogoro huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.