Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Somalia: Makubaliano yafikiwa kuandaa uchaguzi ndani ya siku 60

Siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble na wakuu wa majimbo matano yanayojitawa walitia saini makubaliano ya kufanya uchaguzi "huru na wa haki". 

Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble, Septemba 23, 2020.
Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble, Septemba 23, 2020. AFP - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika kati ya mwezi Desemba 2020 na mwezi Februari 2021 lakini tofauti kati ya vyama mbalimbali zilichelewesha uchaguzi huo, na kuiingiza Somalia katika mgogoro wa kisiasa.

Katikati ya mwezi wa Aprili, kuongezwa kwa muhula wa Rais Mohamed Farmajo, ambao ulimalizika Februari 8, kulisababisha mapigano makali katika mji mkuu Mogadishu. Mwanzoni mwa mwezi Mei, rais alikuwa alijirudi na kuachana na hatua ya kujiongezea mluhula wake, akikabidhi mchakato wa uchaguzi kwa Waziri wake Mkuu.

Pande zinazokinzana zafikia makubaliano

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Somalia aliongoza majadiliano ya faragha, yaliyoanza Mei 22, ambayo yaliwezesha kufikiwa kwa makubaliano yaliyosainiwa Alhamisi, Mei 27

Kupitia makubaliano haya, mamlaka nchini Somalia iliwasilisha njia bora ya kuandaa uchaguzi huo. Hatua ya kwanza ni kukamilisha katiba ya kamati ya uchaguzi ifikapo kesho Jumapili.

Halafu, uchaguzi utalazimika kufanyika ndani ya siku 60 kulingana na ajenda iliyoainishwa baadaye na kamati ya uchaguzi. Uchaguzi huo utafanyika kulingana na mfumo wa moja kwa moja wa uchaguzi ambapo wajumbe maalum, waliochaguliwa na koo, watapiga kura kwa kuwachaguwa wabunge. Wabunge ambao hwatamchagua rais. Kulingana na makubaliano hayo, kila eneo linalojitawala litachagua maeneo mawili ya uchaguzi huu.

AU na Umoja wa MAtaifa kusaidia Somalia

Waziri Mkuu wa Somalia pia ametaka idadi ya 30% ya wanawake watakaochaguliwa kwa bunge iheshimishwe.

Makubaliano hayo yamekaribishwa na kupongezwa na wapinzani na jamii ya kimataifa, kwani mivutano katika miezi ya hivi karibuni ilisababisha hofu ya kuongezeka kwa vurugu.

Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ulaya, pamoja na wengine, wamesema wako tayari kusaidia Somalia "kutunza makubaliano haya ya kihistoria." Rais Farmajo alimshukuru Waziri  wake Mkuu, akisifu jukumu lake la uongozi katika mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.