Uchaguzi nchini Somalia kufanyika baada ya siku 60
Serikali ya Somalia imetangaza kuwa uchaguzi uliocheleweshwa sasa utafanyika ndani ya siku 60 zijazo, baada ya maelewano kati ya wanasiasa na wadau mbalimbali katika taifa hilo la pembe ya Afrika.
Imechapishwa:
Uamuzi huu umekuja baada ya kutamatishwa kwa mazungumzo ya kisiasa ambayo yamekuwa yakiendelea wiki hii mjini Mogadishu.
Waziri wa Habari Abdirahman Yusuf ametangaza kuwa baada ya mashauriano hayo, imekubaliwa kuwa uchaguzi huo ufanyike ndani ya miezi miwili, na sasa tarehe kamili itatolewa na Tume ya Uchaguzi.
Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble amesema ni hatua ya kihistoria na pande zote zimekubaliana kuwa wajumbe maalum waliochaguliwa na wazee wa koo mbalimbali, watawachagua wabunge ambao, watamchagua rais.
Accompanied by Heads of Federal Member States & Benadir Governor, I met the Swedish Foreign Minister for Intl Dev’t Cooperation, Per Olsson Fridh @thinkper, a key dev’t partner that welcomed our Electoral deal. I thanked him for our enduring partnership. pic.twitter.com/6U1AeYMgwg
— Mohamed Hussein Roble (@MohamedHRoble) May 27, 2021
Uchaguzi huu ulitarajiwa kufanyika mwezi Februari lakini serikali inayoongozwa na rais Mohamed Abdullahi Farmajo ikashinswa kuelewana na viongozi wa majimbo matano kuhusu namna ya kuufanikisha.
Hali hiyo ilizua sintofahamu ya kisiasa nchini humo na kufanya mambo kuwa mabaya ziadia baada ya wabunge kupitisha mswada wa kumwongeze muda wa miaka mliwili raius Farmajo, kitendo kilichoolaniwa na wanasiasa wa upinzani.