Pata taarifa kuu
GUINEA

Watu 15 waangammia katika mgodi wa dhahabu ulianguka karibu na Siguiri

Watu wasiopungua kumi na tano wawamefariki dunia Jumamosi, Mei 8, katika maporomoko ya udongo kwenye mgodi wa dhahabu, karibu na mji wa Siguiri, mkasa wa hivi karibuni wa uchimbaji dhahabu ulitokea kaskazini mashariki mwa Guinea.

Mgodi wa dhahabu barani Afrika (picha ya kumbukumbu).
Mgodi wa dhahabu barani Afrika (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO/WHO/PIERRE FORMENTY
Matangazo ya kibiashara

Maporomoka hayo ya udongo yalitokea ghafla wakati wachimbaji katika mgodi huo walikuwa hawana hofu ya kutokea jambo lolote baya dhidi yao.

Maelfu ya wachimba dhahabu haramu wanaokabiliwa na shida kubwa za kuishi, wanakuja kufanya sughuli hiyo katika mji huo wa Siguiri kutoka nchi zote jirani.

Mwamba mrefu ndio ulisababisha maporomoko ya udongo katika mji wa Tatakourou, karibu na mji wa Doko, karibu na mpaka wa Mali. Mwamba ulivunjika kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.

Tukio hili linatokea baada ya mfululizo wa ajali zingine kama hizo ambazo zilisababisha vifo kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.

Miili 15 ilifukuliwa na waokoaji kabla ya kuzikwa mapema jioni. Wanawake wawili ni miongoni mwa watu waliofariki dunia.

Rais wa Guinea Alpha Condé alisema "amehuzunishwa na tukio hilo", kulingana na msemaji wake. Aliiomba serikali ifanye uchunguzi unaohitajika ili kujua sababu hasa za mkasa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.