Pata taarifa kuu
GUINEA-EBOLA

Guinea yakumbwa na mlipuko mpya wa Ebola, wanne wafariki dunia

Nchini Guinea, karibu miaka mitano baada ya kumalizika kwa ugonjwa wa Ebola ulioua zaidi ya watu 11,000 kati ya mwaka 2013 na 2016, virusi hivyo vimezuka tena.

Guinea yatangaza kukumbwa na maambukizi mapya ya virusi vya Ebola.
Guinea yatangaza kukumbwa na maambukizi mapya ya virusi vya Ebola. REUTERS/Baz Ratner/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kesi saba zimethibitishwa kusini mwa nchi, ikiwa ni pamoja na vifo vinne. Idara ya afya ya taifa imesema watu hao walianza kuugua huku wakiendesha, kutapika na kuvuja damu baada ya kuhudhuria mazishi kwenye wilaya ya Goueke.

Idara hiyo pia imeongeza kusema kuwa awamu nyingine ya vipimo inaendelea ili kuthibitisha maambukizi hayo ya virusi vya Ebola na wafanyakazi wa huduma za afya tayari wanawafuatilia watu wote waliokutana na wagonjwa hao

Jumapili Februari 14 mamlaka nchini humo ilikutana katika kikao cha dharura jijini Conakry ili kutafakari kwa makini kuhusu mbinu za kukabiliana na mlipuko huo.

Mkutano huo ulifanyika mbele ya Waziri wa Afya, mamlaka ya kitaifa ya usalama wa Afya (ANSS), Taasisi ya kitaifa ya Afya ya Umma na pia washirika ambao ni Umoja wa Mataifa, shirika la Afya Duniani (WHO), MSF, Alima, CDC, Shirika la Msalaba Mwekundu na wengine. "Guinea inakumbwa na milpuko mpya wa janga la Ebola," amesema Dkt Sakoba Keïta, mkurugenzi wa mamlaka ya kitaifa ya usalama wa Afya (ANSS).

Hatua za dharura zimesitishwa, kama vile kuanza kwa itifaki ya matibabu, huku hatua kadhaa zikichukumiwa. Kutokana na ukosefu wa chanjo nchini humo mamlaka imeamua kuagiza chanjo haraka iwezekanavyoili kukabiliana ugonjwa huo.

Mamlaka pia iliafikiana kutuma timu ya pili ya matabibu na viongozi serikalini katika mji mkuu wa

jimbo la Forest Guinea,Nzérékoré, kusini mashariki mwa nchi, ambayo ilitarajiwa kuondoka Jumapili Februari 14 ili kutenga eneo la maambukizi na kutambua watu waliotangamana na wagonjwa.

Msitu Guinea uliathirika na ugonjwa huo katika miaka ya hivi karibuni

Nzérékore ni mji mkuu wa jimbo la Forest Guinea, jimbo la kusini mwa nchi, ambapo janga hilo lilianza mnamo mwaka 2016 na ambapo kesi hizi mpya ziliripotiwa Jumamosi, Februari 13.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.