Pata taarifa kuu
UNSC-KENYA-DHIBOUTI-USALAMA

Kenya na Djibouti kuchuana kutafuta nafasi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Kenya na Djibouti zinatarajia leo Alhamisi kuchuana katika duru ya pili kutafuta nafasi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambayo imetengewa Afrika, baada ya kutopatikana mshindi Jumatano wiki hii.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakuna kwenye makao makuu ya baraza hilo huko New York, Februari 28, 2020.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lakuna kwenye makao makuu ya baraza hilo huko New York, Februari 28, 2020. REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo wajumbe 4 wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamechaguliwa katika Mkutano mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

India, Mexico, Norway na Ireland zimebahatika kuchaguliwa kuhudumu kwa muda wa miaka miwili 2021 na 2022, katika Baraza kuu la Usalama la umoja huo. India na Mexico ziliwania nafasi zao bila kuwa na upinzani.

Wakati huo huo Kenya na Djibouti zinatarajia leo Alhamisi kuchuana katika duru ya pili kutafuta nafasi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambayo imetengewa Afrika.

Mshindi hakupatikana kati ya Kenya na Djibouti baada ya kushindwa kupata theluthi mbili ya kura zinazohitajika. Kenya na Djibouti sasa zitachuana katika baraza hilo mjini New York.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina wanachama 15, watano kati yao ni wa kudumu na kumi sio wa kudumu. Nafasi za kifahari ambazo zinaweza kuwezesha baadhi ya nchi kuendeleza ajenda zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.