Pata taarifa kuu
DJIBOUTI-CORONA-AFYA

Djibouti yatangaza visa vipya 156 vya maambukizi ya Covid-19

Djibouti imeripoti visa 156 vya maambukizi ya virusi vya  Corona katika saa 24 zilizopita na kuongeza idadi yote ya wagonjwa kufikia 591, hii ikiwa idadi kubwa katika pembe ya Afrika.

Moja ya mitaa ya mji wa Djibouti, mwaka 2016 (picha ya zamani).
Moja ya mitaa ya mji wa Djibouti, mwaka 2016 (picha ya zamani). Flickr.com CC BY 2.0 Francisco Anzola
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya Mohammed Warsame aidha amethibitisha vifo vya watu wawili kutokana na ugonjwa huo, huku watu 73 wakiripotiwa kupona.

Virusi vya Corona vinaendelea kusambaa ulimwenguni, na tayari vimeathiri uchumi katika nchi mbalimbali duniani.

Nchi nyi zimechukuwa hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo hatari, ambao Umoja wa Mataifa uliuta janga la kimataifa.

Nchi zaidi ya 182 zinaendelea kukumbwa na ugonjwa huo wa Covid-19.

Barani Afrika nchi zaidi ya 40 zinaendelea kukabil na ugonjwa wa Covid-19, ambapo watu zaidi ya 17,000 wameambukizwa virusi vya Corona, kulingana na ripoti za chuo kikuu cha Marekani cha Johns-Hopkins, ambacho kinatoa taarifa kwa kila nchi kuhusu ugonjwa wa Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.