Pata taarifa kuu

Watu sitini waangamia katika mapigano ya kijamii Darfur

Zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa katika mauaji mapya yaliyotokea katika kijiji kilichopo Magharibi mwa Darfur kulingana na Umoja wa Mataifa.

Mapigano ya mara kwa mara yamesababisha watu wengi kuyahama makazi yao na kukimnilia maeneo salama; Hapa ni katika kambi ya Umoja wa Mataifa ya Kalma (Darfur Kusini).
Mapigano ya mara kwa mara yamesababisha watu wengi kuyahama makazi yao na kukimnilia maeneo salama; Hapa ni katika kambi ya Umoja wa Mataifa ya Kalma (Darfur Kusini). AFP PHOTO/UNAMID/ALBERT GONZALEZ FARRAN
Matangazo ya kibiashara

Mfululizo wa mashambulio yameendelea tangu wiki iliyopita kati ya makabila yenye kuhama-hamaya ya Kiarabu na wakulima wasio Waarabu kuhusu umiliki wa ardhi.

Kulingana na umoja aw Mataifa, karibu watu 500 wenye silaha walishambulia mji wa Masteri siku ya Jumamosi, kama kilomita hamsini kutoka mji mkuu wa mkoa wa El Geneina. Zaidi ya watu 60 waliuawa, wengi ni kutoka jamii ya Massalit. Nyumba na soko la eneo hilo pia vilichomwa moto baada ya visa vya uporaji kuripotiwa.

Kwa siku kadhaa, machafuko mabaya ya kikabila yameongezeka katika eneo hilo. Siku ya Ijumaa, watu wasiopungua 20 waliuawa huko Darfur Kusini.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Abdallah Hamdok ameahidi katika taarifa "kwamba kikosi cha pamoja cha usalama, kinachojumuisha polisi na jeshi, kitatumwa katika majimbo matano ya Darfur ili kuhakikisha usalama wa raia umeimarishwa vilivyo na kulinda msimu wa kilimo" uambao unadumu tangu mwezi Julai hadi Novemba.

Katika miaka ya hivi karibuni, mzozo kati ya Waarabu na wasio Waarabu umepungua kwa kiwango kikubwa huko Darfur, lakini suala la ardhi limeendelea kusababisha machafuko. Na mivutano hii bado inahatarisha majaribio ya mazungumzo kwa minajili ya mkataba wa amani kati ya Khartoum na makundi mbali mbali ya waasi, ikiwa ni pamoja na yale ya Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.