Pata taarifa kuu

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1989: Omar al-Bashir akabiliwa na adhabu ya kifo

Kesi mpya inayomkabili aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir inaanza Jumanne hii, Julai 21. Omar al-Bashir aliondoka madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Aprili 2019.

Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir akiwa Mahakamani, Khartoum, Agosti 31, 2019.
Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir akiwa Mahakamani, Khartoum, Agosti 31, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Omar al-Bashir alihukumiwa mnamo mwezi Desemba mwaka jana kifungo cha hadi miaka miwili kwa kosa kosa la rushwa.

Hata hivyo Omar al-Bashir anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama kujibu tuhuma zinazohusiana na jaribio la mapinduzi la mwaka 1989.

Mapinduzi ya Omar El Bashir yalifanyika mwaka 1989 dhidi ya Sadiq al-Mahdi, Waziri Mkuu wa wakati huo wa Sudan na kushika hatamu za uongozi wa nchi.

Baada ya al-Bashir kuiongoza Sudan kwa mkono wa chuma kwa miaka 31, sasa anatarajia kujibu tuhuma zinazomkabili mbele ya mahakama maalumu inayoundwa na mkuu wa Mahakama Kuu na majaji wawili kutoka Mahakama Rufaa.

Anatuhumiwa kukiuka agizo la katiba na anakabiliwa na adhabu ya kifo. Omar al-Bashir atahukumiwa na watu wengine 16, raia wa kawaida na askari, akiwemo Makamu wa Rais Taha na Jenerali Bakri Hassan Saleh.

Hata hivyo Mohamed Al Hassan Al Amin, mmoja wa wanasheria wa Omar al-Bashir, anaema kesi dhidi ya mteja wao ni ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.