Pata taarifa kuu
SUDANI-USALAMA-SIASA

Mawaziri sita wajiuzulu nchini Sudan

Mawaziri sita nchini Sudan wamejiuzulu na mmoja kufutwa kazi, baada ya maelfu ya watu hivi karibuni kuandamana nchini humo wakishinikiza mageuzi yaliyoahidiwa baada ya uundwa kwa seriklai ya mpito nchini humo.

Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok.
Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok. Ebrahim HAMID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri mkuu  Abdallah Amdok amesema  walioondoka ni pamoja  na waziri wa mashauriano ya kigeni,fedha,uchukuizi, kilimo na nishati ,huku waziri wa afya akiwa amefutwa kazi.

Katika hatua nyingine, serikali ya mpito na makundi ya waaasi yanayoendelea na mazungumzo ya Amani katika nchi jirani ya Sudan Kusini, wamekubaliana kutia saini makubaliano ya mazungumzo hayo katika kipindi cha majuma mawili yajayo.

Mwezi uliopita Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita ya ICC, iliwataka washukiwa inayowatafuta kutoka nchini Sudan kujisalimisha haraka iwezekanavyo, kabla hawajakamatwa na vyombo husika na kupelekwa Hague, makao makuu ya mahakama hiyo ya kimataifa.

Hatua hii imekuja siku moja baada ya mshukiwa mmoja Ali Kushayb kujisalimisha katika Mahakama hiyo yenye makao yake jijini Hague nchini Uholanzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.