Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Spika la Bunge wa Libya atoa wito kwa Misri kutuma jeshi ikiwa mji wa Sirte utavamiwa

Spika wa bunge la Libya liloko eneo la mashariki mwa nchi hiyo Aguila Saleh, ameitaka Misri kutuma majeshi yake, iwapo wapiganaji wanaoungwa mkono na serikali ya umoja wa kitaifa inaotambuliwa kimataifa,watashambulia mji wa Sirte ambayo ni ngome yake.

Spika wa Bunge la Libya Aguila Saleh,Benghazi Aprili 13, 2019.
Spika wa Bunge la Libya Aguila Saleh,Benghazi Aprili 13, 2019. Abdullah DOMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Misri inawaunga mkono wanajeshi wa upinzani wanaongoza na Jerali Khalifa Haftar na wito huu unakuja, baada ya Umoja wan chi za kiarabu kuomba usitishwaji wa mapigano nchini humo.

Hivi karibuni serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa ililaani kile ilichokitaja kuwa ni matamshi ya vitisho vya vita dhidi ya Libya yaliyotolewa na rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi.

Akizungumza punde baada ya kukikagua kituo cha jeshi la wanamaji, kilichoko karibu na eneo la mpakani kati ya Misri na Libya mwishoni mwa juma lililopita, rais wa Misri, Abdel Fattah al Sisi alisema kuwa nchi yake ina haki ya kuingilia moja kwa moja katika mzozo unaolikumba taifa jirani la Libya.

Wakati huo huo msemaji wa jeshi la Libya (GNA) Mohammed Gununu, aliandika kwenye mtandao wa Twitter akimjibu rais wa Misri kwamba: “Libya haijawahi kutishia usalama wa nchi jirani, na kwamba wako tayari kujibu mashambulkizi yoyote kutoka nje ya taifa hilo”. 

Mapema wiki hii Mataifa yanayounda Umoja wa Kiarabu yametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuacha kuingilia kati masuala ya Libya, na kutaka pia kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini humo.

Umoja wa nchi za Kiarabu uliunga mkono msimamo wa Misri wa kutaka kuvunjwa kwa wanamgambo na kuowaondoa mamluki nchini Libya na hivyo kurahisishia mkataba wa kusitisha mapiganouliofikiwa hivi karibuni kati ya pande hasimu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.