Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Chad yaamua kuendeleza operesheni zake dhidi ya wanajihadi

Serikali ya Chad imetangaza kwamba jeshi lake litaendelea kushiriki katika juhudi za kikanda za kupambana dhidi ya makundi ya wanajihadi na ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, baada ya kauli ya Rais Idriss Deby iliyozua sintofahamu.

Raisa wa Chad, Idris Deby, Aongoza mapambano dhidi ya Boko Haram.
Raisa wa Chad, Idris Deby, Aongoza mapambano dhidi ya Boko Haram. wotzup.ng
Matangazo ya kibiashara

Katika video iliyotolewa Ijumaa wiki iliyopita, rais wa Chad alisema kuwa wanajeshi wa Chad waliuawa wakiwa katika shughuli ya kulinda amani katika "Ziwa Chad na kwa eneo nzima la Saheli" na kutangaza kwamba "kuanzia leo hakuna mwanajeshi wa Chadi atakayeshiriki [ katika operesheni za kijeshi nje ya Chad. "

Maneno hayo "yalitafasiriwa vibaya," alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje siku ya Jumapili.

"Chad haijawahi kutamka kuwa "itajiondoa katika kikosi cha mseto cha jeshi la kimataifa (FMM) kilichoundwa dhidi ya Boko Haram, wala kutoka kwa jeshi la pamoja la G5 Sahel au kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, alisema katika taarifa.

Chad, ambayo jeshi lake linachukuliwa kuwa lenye ubora na nguvu zaidi katika ukanda huo, ni moja wa nchi muhimu katika mapambano dhidi ya makundi ya kijihadi huko Sahel na karibu na Ziwa Chad na ni mmoja ya wachangiaji wakuu katika ujumbe wa kudumisha amani nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.