Pata taarifa kuu
CHAD-SENEGAL-HABRE-CORONA-AFYA-HAKI

Senegal: Hissène Habré aondolewa jela kwa muda

Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré anakutana na familia yake tangu Jumatau joni wiki hii baada ya kuondolewa jela, uamuzi ulitochukuliwa na mahakama nchini Senegal.

Hissène Habré akizungukwa na askari baada ya kusikilizwa mahakamani, Julai 2, 2013 huko Dakar.
Hissène Habré akizungukwa na askari baada ya kusikilizwa mahakamani, Julai 2, 2013 huko Dakar. © AFP/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Hissène Habré ameondolewa jela kwa siku sitini, ili kuepuka asiwezi kuambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 katika jela ambako alikuwa akizuiliwa.

Hissène Habré ni miongoni mwa watu ambao ni raihisi kupata virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Cpvid-19 kutokana na umri wake mkubwa. Kiongozi huyo wa zamani wa Chad ana umri wa miaka 77.

Akihojiwa na RFI, mkewe Hissène Habré, Fatimé Raymonde Habré, amethibitisha kuondolewa jela kwa mumewe, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

"Sio kukuachiliwa huru, lakini badala yake ameondolewa jela chini ya ulinzi mkali na atabaki siku sitini akiwa katika kifungo cha nyumbani, " mamlaka ya magereza imebaini katika taarifa.

Hissène Habré alikuwa anatumikia kifungo chake cha maisha jela katika jela la Cap Manuel, nchini Senegal, baada ya kuhukumiwa katika Mahakama ya Rufaa mwaka wa 2017 kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa utawala wake nchini Chad kati ya mwaka 1982 na 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.