Pata taarifa kuu
CHAD-UCHUMI-USALAMA

Askari sita wa Chad wauawa katika shambulio jipya

Jeshi la Chad linaendelea kulengwa katika mashambulizi mbalimbali yanayotekelezwa na makundi ya watu wenye silaha, huku raia wakiendelea kuhofia usalama wao.

Jeshi la Chad likipiga doria katika Jimbo la Biltine.
Jeshi la Chad likipiga doria katika Jimbo la Biltine. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Askari sita waliuawa Jumatatu katika shambulio jipya linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram karibu na Kisiwa cha Tetewa, kinachopatikana kwenye Ziwa Chad, eneo ambalo machafuko yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

"Askari wetu walikuwa wanapiga doria wakati walishambuliwa na wanamgambo wa Boko Haram. Tunasikitishwa na vifo vya askari sita waliouawa na kumi kujeruhiwa," Jenerali Taher Erda, mkuu wa majeshi ya Chad ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Vikosi vyetu vilikuwa vinawasaka wanamgambo wa Boko Haram wakati waliposhambuliwa na adaui karibu na eneo la Mandrari, mahali panakozungukwa na nyasi refu," ofisa wa eneo hilo, ambaye hakukataa kutajwa jina, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa miezi kadhaa, wanamgambo wa Kiislamu wameongeza mashambilizi karibu na Ziwa Chad, eneo kubwa la visiwa lililojaa maji kwenye mpaka wa Chad, Cameroon, Niger na Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.